SIMBA WANAWEZA KUMKOSA BOCCO KWENYE NGAO YA JAMII
Baada ya Simba kulazimishwa matokeo ya 0-0 katika mchezo wa jana dhidi ya Namungo, habari mbaya kiasi kwa Wanasimba ni kuw anahodha wao John Bocco bado ni majeruhi.
Simba inatarajiwa kushuka uwanjani baadaye mwezi huu kukipiga dhidi ya Mtibwa Sugar katika Ngao ya Hisani jijini Mwanza na kuna uwezekano mkubwa wa staa huyo kuukosa mchezo huo.
Mtanange huo wa Ngao ya Hisani utapigwa Agosti 18 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na tayari presha imeanza kuwa kubwa kwa Simba kwa kuwa licha ya kutumia kiasi kikubwa kusajili na kuweka kambi nchini Uturuki, bado timu hiyo haijapata ushindi katika michezo miwili iliyopita ya kujipima nguvu.
Bocco aliukosa mchezo wa kirafiki dhidi ya Asante Kotoko Agosti 8 katika tamasha la Simba Day ambalo lilimalizika kwa sare ya bao 1-1 pamoja na jana dhidi ya Namungo FC huko Ruangwa, Lindi.
Comments
Post a Comment