MABAO 9 YA KAGERE YAWATIKISA YANGA



Meddie Kagere.
KASI ya ufungaji wa mabao ya Meddie Kagere siyo kwamba inawafurahisha Simba tu, imewatia tumbo joto Yanga licha ya kwamba wanabeza.

Alichofanya straika huyo raia wa Rwanda kwenye mechi ya ligi dhidi ya Mbeya City alipofunga mabao mawili ya vichwa kiliwaamsha mashabiki wa Simba lakini kwenye jukwaa la Yanga na penyewe kuliibuka mi­jadala juu ya ufundi wake.

Mabao hayo ambayo yalifungwa kiufundi kwenye engo ngumu, yaliwafikirisha mashabiki wa Yanga ambao muda mwingi walikuwa kwenye vikundi wakimjadili zaidi mchezaji huyo ingawa walijipa matumaini kwamba Mkongomani wao, Heritier Makambo naye ni tishio.
Mchezaji, mwanachama na kocha wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ alisema; “Kagere ni mchezaji mzuri ambaye ni wazi anajua kupambana hata suala la ufungaji ma­bao siyo ajabu, sasa uw­ezo wake uwanjani sio wa kubeza lakini Makambo yeye nimemuona kwenye mechi moja, kama ataen­delea vizuri basi atakuwa mchezaji mzuri sana.”

Kagere mpaka sasa amefunga mabao matatu kwa kichwa kwenye michezo miwili tofauti ule dhidi ya Mbeya City amefunga mabao mawili kwa kichwa na ule dhidi ya Singida United kwenye Kagame huku mpinzani wake ambaye ni Makam­bo akiwa na bao moja la kichwa ingawa hajacheza mechi nyingi kama Kagere.

Kagere ambaye ameu­pumzisha kwa muda umahiri wa Emanuel Okwi na John Bocco, amefunga mabao tisa mpaka sasa ndani ya Simba katika michuano tofauti ile ya Kagame 2018, ligi pamoja na mechi za kirafiki ambazo amecheza tangu asajiliwe na Mohammed Dewji ‘MO’.

Makambo amesajiliwa hivi karibuni na Yanga na tayari amefunga mabao manne ambayo alifunga dhidi ya Mawenzi Market, Tanzanite Academy na dhidi ya USM Alger na Mtibwa Sugar.

Kwa upande wa Okwi kinara wa mabao ya msimu uliopita mechi za kirafiki ana mabao matatu na ligi hajacheza kutokana na kuwa maje­ruhi.

Licha ya kasi hiyo ya Kagere ya mabao ya kichwa lakini mfalme wa vichwa mpaka sasa ni Mrundi Amissi Tambwe ambaye msimu uliopita alishindwa kutamba na msimu huu unaanza rekodi yake ataendelea nayo au tayari anamkabi­dhi Kagere.

Kumbuka mbali na mechi hizi Kagere pia ali­funga kwa kichwa wakati akiwa na Gor Mahia dhidi ya Simba kwenye mechi ya Sport Pesa na ame­wahi kufanya hivyo dhidi ya Yanga kwenye kombe la Shirikisho Afrika

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!