Jeshi’ la Yanga linaendelea na kambi yake ya kujiandaa kwa ajili ya msimu wa 2018/19 ambapo mazoezi yamekuwa ni ya nguvu mkoani Morogoro.
Mbali na kujiandaa na msimu mpya, timu hiyo pia inajiandaa kwa mchezo ujao dhidi ya Waarabu, USM Alger katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa Agosti 19 jijini Dar es Salaam.
Yanga imefanya vibaya katika michuano hiyo ambayo ipo hatua ya makundi lakini chini ya kocha wao, Mwinyi Zahera kila kitu kinaonekana kwenda vizuri.
Pichani ni wakati wa mazoezi ya timu hiyo ambayo ipo kambini mkoani Morogoro.
Comments
Post a Comment