Simba watua Tanga kibabe



Dar es Salaam. Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara wamewasili jijini Tanga kukipiga na maafande wa JKT Tanzania mchezo ambao utapigwa Uwanja wa Mkwakwani keshokutwa Jumamosi.
Simba ambao wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara na pointi 23, chini ya Yanga iliyo ya pili na pointi 25 na vinara wakiwa ni Azam FC yenye 27.
Waliondoka Asubuhi mapema tayari kuwavaa maafande hao ambao pia ni tishio, wapo kwenye nafasi ya tano na pointi 18, baada ya kucheza mechi 11.
Mratibu wa Simba, Abbas Ally amesema, timu imewasili salama Tanga na wanafanya maandalizi mengine kwa ajili ya mchezo huo.
"Tumefika salama Tanga na sasa tunafanya mipango ya kuwaweka sawa wachezaji wetu na mambo mengine yote yanakwenda sawa tayari kwa mchezo,"alisema Abbas. 
Simba ni mgeni wa JKT Tanzania ambayo imeuchagua Uwanja wa Mkwakwani kuwa wao wa nyumbani pamoja na ule wa Meja Jenerali Isamuhyo wa Dar es Salaam.
Imepanda Ligi Kuu msimu huu pamoja na timu za Alliance FC ya Mwanza, African Lyon na KMC za Dar es Salaam, Coastal Union ya Tanga na Biashara United ya Mara.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!