MADRID WAMFUATA RASHFORD ENGLAND



KLABU ya Real Madrid im­eonekana kuweka nguvu yake kwenye usajili kwa sasa baada ya kutenga kitita cha pauni milioni 90 (zaidi ya shilingi bilioni 200), kwa ajili ya kumsa­jili Marcus Rashford wa Man United na Christian Eriksen wa Tottenham Hotspur.

Madrid hawapo kwenye kiwango kizuri zaidi kwa sasa na wanatakiwa kuhakikisha wanafanya usajili kabambe ili kujiwek a kwenye mazingira mazuri ya kutwaa makombe msimu huu.
Mabosi wa Real Madrid walikuwa uwanjani kumtazama mshambuliaji Rashford wakati akiichezea England ilipokuwa ikivaana na Croatia kwenye Dimba la Wembley.

Madrid wanaamini kuwa mshambuliaji huyu anaweza kuziba pengo la Cristiano Ronaldo ambaye aliondoka kwenye timu hiyo na kujiunga na Juventus.
Madrid ambao ndiyo mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya pia wanamtaka kiungo wa Spurs, Eriksen kwa ajili ya kuziba pengo la Luka Modric ambaye wanaamini kuwa mwishoni mwa msimu huu anaweza kuondoka kwenye timu hiyo.

Kocha wa United, Jose Mourinho ameonekana kama vile hamkubali Rashford na mchezaji huyo ameanza kwenye michezo mitano tu ya Ligi Kuu England msimu huu.
Hii inaweza kuwa nafasi pekee kwa kinda huyo kuondoka na kujiunga na Madrid ambayo inaweza kumpa nafasi ya kutosha kwenye kikosi cha kwanza.

Wakati Madrid wakitenga kitita cha pauni milioni 50, kwa ajili ya Rashford wametenga pauni milioni 40 kwa ajili ya Eriksen ambaye amekuwa akionyesha uwezo wa juu sana uwanjani.
MADRID, Hispania

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!