MASTAA 5 WALIOTWAA TAJI LA LIGI YA UEFA WAKIWA NA TIMU 2 AU ZAIDI



KILELE cha sifa katika soka la klabu barani Ulaya ni kushiriki na kutwaa taji la  Ligi ya Ubingwa ya UEFA (UCL).  Makocha na wachezaji wengi hulichukulia taji la ligi hiyo kuwa linashika nafasi ya pili duniani kwa heshima baada ya Kombe la Dunia.
Baadhi ya wanasoka wakubwa duniani wameshinda mataji ya UCL ambao ni pamoja na  Ronaldo na Gianluigi Buffon.
Wengine ni Messi, Andries Iniesta, Iker Casillas na Paulo Maldini ambao wamelitwaa japo kwa klabu moja tu.  Wafuatao ni wachezaji watano walioshinda taji hilo wakiwa na klabu zaidi ya moja.

Related image

Clarence Seedorf : Mholanzi huyo alishinda kombe hilo mara ya kwanza akiwa na klabu ya Ajax Amsterdam msimu wa 1994/1995, akalitwaa tena akiwa na Real Madrid mnamo 1997/1998. Mara ya tatu alishinda akiwa na AC Milan mnamo 2002. Kiungo huyo aliisaidia Milan mara mbili, mnamo 2003/ 2004 na 2006/ 2007.

Image result for Samuel Eto’o
2. Samuel Eto’o,   mshambuliaji wa  Cameroon, alikuwa ni mmoja wa washambuliaji waliokuwa wanaogopewa zaidi barani Ulaya hususan alipokuwa bado kijana mbichi.  Eto’o alilitwaa taji la UCL  mara mbili akiwa na Barcelona, kwanza mnamo 2005/ 2006 akilingana na Leo Messi na Ronaldinho. Alilitwaa tena mnamo  2008/ 2009 na msimu uliofuata alilitwaa akiwa na Inter Milan chini ya Jose Mourinho. 
Image result for Marcel Desailly

3. Marcel Desailly, mlinzi mwenye nguvu nyingi wa Ufaransa, aliitwaa akiwa na klabu ya Marseille mnamo  1992/ 1993, kisha akiwa na AC Milan, msimu uliofuata mwaka 1994 walipowashinda Barcelona.

Image result for Cristiano Ronaldo


4. Cristiano Ronaldo, ambaye huenda ni mmoja wa wanasoka mahiri zaidi duniani kwa sasa, alianza kulitwaa msimu wa 2007/ 2008 akiwa na Manchester United, akaenda Real Madrid iliyolitwaa msimu wa  2013/ 2014. Madrid iliendelea kulitwaa taji hilo misimu mitatu mfululizo kutoka 2015 hadi 2018. Ronaldo anategemea kuungana na Seedorf kulitwaa taji hilo mara tatu katika klabu tofauti ambapo sasa yuko  Juventus.

Image result for Toni Kroos Kroos

5. Toni Kroos Kroos,  kiungo mahiri wa Ujerumani, alianza kulitwaa taji hilo msimu wa  2012/ 2013 akiwa na Bayern kabla ya kwenda Madrid na kulitwaa misimu mitatu mfululizo akiwa na Ronald. Ni Mjerumani pekee aliyelitwa taji hilo na klabu mbili tofauti.


Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!