KAPOMBE APASULIWA MGUU SAUZ
BEKI wa kulia wa Simba, Shomari Kapombe, amefanyiwa upasuaji wa mguu kufuatia kuumia enka kwenye kambi yaTaifa Stars nchini Afrika Kusini.
Beki huyo alikuwa kwenye kambi ya timu hiyo iliyokuwa inajiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu Afcon dhidi ya Lesotho katika mchezo uliopigwa nchini Lesotho, wikiendi iliopita.
Beki huyo ambaye alilazimika kubakia nchini humo kwa ajili ya kupatiwa matibabu, juzi alifanyiwa upasuaji wa mguu wake katika hospitali moja kubwa kwenye Jiji la Pretoria, Afrika Kusini.
Akizungumza na Championi Jumatatu, mwenyekiti wa timu hiyo, Swedy Mkwabi alisema upasuaji huo utamlazimu Kapombe kukaa nje ya uwanja kwa wiki sita.
“Kesho Jumatatu (leo) atakwenda tena hospitali kuonana na daktari wake ili kuangalia maendeleo baada ya upasuaji kwa sababu atakuwa nje kwa muda wa wiki sita isipokuwa atarejea nchini wakati wowote kulingana na daktari wake atakavyokuwa ameongea naye,” alisema Mkwabi.
WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam
Comments
Post a Comment