MAN U YATAYARISHA BN. 77 KUMCHUKUA PELLEGRINE WA ROMA


Lorenzo Pellegrini
Manchester United ya Uingereza wanatayarisha kitita cha Pauni Bil. 26 kumchukua kiungo wa timu ya Roma ya Italia, Lorenzo Pellegrini, mwezi Januari mwaka ujao huku timu yake hiyo ikitia ngumu kutomwachia kirahisi.
Kocha Jose Mourinho wa Man U ambaye ni kipenzi mkubwa wa soka la Pellegrini (22) anayechezea pia  timu ya taifa ya Italia, anataka kumnasa na kumwongeza mshahara wake wa Paundi 890,000 kwa mwaka, kuwa mara mbili; yaani ufikie Sh. bil. 6.7.
Gazeti la michezo la  Italia la Corriere dello Sports, limesema wakala wa Pellegrini aitwaye Giacomo Pocetta, alikutana na wakurugenzi wa United jijini Londoni  ambako klabu hiyo ilipendekeza donge hilo nono.


Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!