Manchester Dabi: Wako wapi Mashetani Wekundu tuliowazoea?
IN SUMMARY
Kwa mujibu wa rekodi, Manchester United wanaongoza kwa ubabe, ambapo katika michezo 176 ya Dabi iliyopigwa huko nyuma, Mashetani wekundu walishinda mara 73 na City wameshinda mechi 51 huku michezo 52, zikimalizika kwa sare.
Manchester, England. Leo Usiku, majira ya saa 1:30, saa za Afrika Mashariki, macho na masikio yataelekezwa katika Jiji la Manchester. Shughuli zote zitasitishwa. Maduka yatafungwa. Safari hii shoo ya kibabe inapigwa pale Etihad. Manchester City, wanawaalika mahasimu wao, Manchester United. Patachimbika leo!
Naam, kipute cha mahasimu ndio kimewadia mwanangu. Mwamuzi ameshajulikana. Sio mwengine bali ni mtoto wa nyumbani, uzao wa Jiji la Manchester, Anthony Taylor. Hii ndio mechi yake ya kwanza ya Manchester Dabi. Ila hiyo sio ishu.
Ikiwa ni Dabi ya 177, ulimwengu utamshuhudia, Jose Mourinho akiliongoza jeshi lake kumfuata hasimu wake mkubwa Pep Guardiola kwenye dimba la Etihad kuwania kusaka kama sio pointi tatu basi hata moja, Itawezekana kweli? Rekodi hazidanganyi.
Kwa mujibu wa rekodi, Manchester United wanaongoza kwa ubabe. Katika michezo 176 ya Dabi iliyopigwa huko nyuma, Mashetani wekundu walishinda mara 73 na City wameshinda mechi 51 huku michezo 52, zikimalizika kwa sare.
Kwa sasa Guardiola na jeshi lake, ambalo ndio mabingwa watetezi wa EPL, wanaongoza ligi na pointi zao 29. Hawajapoteza mechi hata moja huku Mourinho akiwa nafasi ya nane na pointi 20.
Pep, anataka kuendeleza rekodi ya ushindi dhidi ya Mourinho, ambaye amekuwa akikutana na wakati mgumu kila wanapokutana tangu wakiwa La Liga. Ataweza? Tusubiri muda uamue.
Pamoja na ukweli usiopingika kwamba, United wanaongoza kwa ubabe kwenye Dabi nyingi, Ikumbukwe kuwa, mechi nyingi zilipigwa katika enzi za ubabe wa Sir Alex Ferguson! Huu ni enzi nyingine na mambo yamebadilika.
Unapowatizama United wanavyocheza, nafasi yao kwenye ligi halafu ukageuka upande wa pili na kuwatizama City, lazima utajiuliza maswali lukuki. Swali la msingi, likiwa ni wako wapi wale mashetani wekundu tuliowazoea?
United wa sasa ni wabangaizaji tu. Mashetani wekundu ambao tulizoea kuwashuhudia wakiwabatiza wapinzani wao kwa moto, pale machinjioni, Old Trafford, siku hizi wanapata tabu sana!
Wazee wa ‘comeback’, wakali wa kufunga bao na kupata ushindi katika dakika za lala salama, siku hizi wako hoi. Nini tatizo, kipi kimetokea hapa katikati? Haya ni maswali magumu yanayozunguka katika vichwa vya wapenda soka, kuelekea mechi ya leo.

Comments
Post a Comment