Okwi, Kagere waibeba Simba kwa Yanga msimamo Ligi Kuu


IN SUMMARY
Sare ya bao 1-1, iliyopata Yanga dhidi ya Ndanda Jumapili iliyopita ndiyo iliyowapa kicheko Simba na kuendelea kusalia katika nafasi ya pili kwenye msimamo.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT
Dar es Salaam. Licha ya Simba na Yanga zote kuwa na pointi 26,safu ya ushambuliaji ya wekundu wa Msimbazi inayoongozwa na Emmanuel Okwi na Meddy Kagere imeonekana kuibeba timu hiyo kwenye msimamo wa ligi.
Mabao 23 iliyofunga Simba mpaka sasa kwenye ligi yamewawezesha kuendelea kuishikilia nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi na kuwa juu ya watani zao Yanga walio nafasi ya tatu licha ya timu hizo zote mbili kuwa sawa kwa pointi 26.
Okwi na Kagere peke yao wamefunga mabao 14 wakizidiwa mawili na timu nzima ya Yanga ambayo imefunga mabao 16.
Hata hivyo sare ya bao 1-1 iliyopata Yanga dhidi ya Ndanda Jumapili iliyopita ndiyo iliyowapa kicheko Simba na kuendelea kusalia katika nafasi ya pili kwenye msimamo.
Kama Yanga ingeshinda siku hiyo basi Simba ingeshuka mpaka nafasi ya tatu.
Hata hivyo Yanga bado ina nafasi ya kuipiku Simba kwani ina mchezo miwili mkononi zaidi ya wekundu hao wa Msimbazi

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!