KAPOMBE KUBAKIA SAUZ
BEKI wa kulia wa Simba, Shomari Kapombe, atalazimika kubakia Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu kufuatia majeraha ya kuvunjika mguu aliyoyapata akiwa na timu ya taifa, Taifa Stars nchini Afrika Kusini.
Kapombe aliumia akiwa kwenye kambi ya timu hiyo iliyokuwa inajiandaa na mchezo wa kufuzu Afcon uliopigwa kwenye Uwanja wa Setsoto hapa Maseru, Lesotho, jana Jumapili.
Taarifa ambazo Championi Jumatatu limezipata kutoka kwa viongozi wa Simba, zinasema kuwa beki huyo atalazimika kubakia Afrika Kusini kwa ajili ya kupatiwa matibabu kwa daktari wake maalum kabla ya kurejea nchini kuendelea na majukumu ya timu yake.
Awali kabla ya kufikia makubaliano juu ya mchezaji huyo kubakia nchini humo, uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ulipanga kumpeleka Dubai kwa ajili ya kupata matibabu hayo lakini viongozi wa Simba waliopo nchini hapa wamependekeza abakie Afrika Kusini kwa kuwa ana daktari wake maalum.
Beki huyo amevunjika mguu karibu na eneo la enka hali ambayo imesababisha aukose mchezo wa jana nchini hapa.
Comments
Post a Comment