NYOTA SERENGETI AFUZU SOKA LA KULIPWA


NAHODHA wa Serengeti Boys, Morice Abraham amefanikiwa kufuzu majaribio yake ya kucheza soka la kulipwa katika klabu ya vijana (U17) ya Midtylland ya Dernmak.

Morice alirejea nchini hivi karibuni akitokea Denmark ambako alikuwa huko kwa majaribio ya wiki mbili na sasa yupo kwenye kambi ya Serengeti inayojiandaa na michuano ya COSAFA itakayofanyika Botswana Desemba, mwaka huu.

Wakati Morice akitusua, Mtanzania mwingine Kelvin John ‘Mbappe’, naye amegeuka kivutio kwa walimu wa timu ya HB Koge ya Denmark ambako anafanya majaribio kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza soka.

Morice amelimbia Championi Jumamosi kuwa, baada ya kurudi nyumbani alipokea taarifa kwa mdomo kuwa amefanikiwa kufuzu majaribio yake na tayari barua ya uthibitisho imemfikia hivyo muda wowote ataelekea Denmark baada ya kukamilisha mipango yake.

“Barua ya majibu imeshakuja na sasa uongozi wangu ukiongozwa na kocha Oscar Mirambo (Kocha wa Serengeti Boys) unafanya utaratibu wa kuangalia nitakwenda kuishi katika mazingira gani, hasa katika suala la elimu kwa kuwa bado sijamaliza masomo hivyo mwalimu anahitaji kufahamu nitasomaje nikiwa kule,” alifunguka Morice.

Kwa upande wa meneja wa Kelvin ambaye yupo naye Denmark, Mbaki Mutahaba amesema mchezaji wake anaendelea vizuri huku walimu wa kituo alichopo wakionyesha kuvutiwa naye kutokana na kufanya kila anachoagizwa na walimu wake.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!