Azam: Simba, Yanga zisahau ubingwa msimu huu



IN SUMMARY
Azam na Yanga ndio timu pekee ambazo hazijapoteza mchezo huku wanalamba lamba hao wakiongoza ligi wakiwa na pointi  30 baada ya kucheza michezo 12,wameshidna tisa na kutoa sare michezo mitatu.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT
Dar es Salaam.Kocha msaidizi wa Azam Fc,Juma Mwambusi amesema mpaka kieleweke msimu huu kwa kuhakikisha wanachukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara bila kupoteza mchezo.
Azam na Yanga ndio timu pekee ambazo hazijapoteza mchezo huku wanalamba lamba hao wakiongoza ligi wakiwa na pointi  30 baada ya kucheza michezo 12,wameshidna tisa na kutoa sare michezo mitatu.
Timu hiyo ndiyo pekee mpaka sasa yenye safu kali ya ulinzi baada ya kuruhusu mabao machache msimu huu ikiwa imefungwa mabao mawili tu ikifuatiwa na JKT Tanzania iliyoruhusu mabao matatu.
Mwambusi alisema licha ya kuongoza ligi na kuendelea kupata matokeo mazuri bado hawajaridhika  mpaka pale watakapokamilisha malengo yao.
Kocha huyo wa zamani wa Yanga na Mbeya City alisema wanachomuomba Mungu ni kuendelea kuwaepusha wachezaji na majeruhi na kuwa na kiwango zaidi ya ilivyo sasa ili mwisho wa msimu watwae ubingwa bila kupoteza mchezo.
Azam itashuka tena dimbani Novemba 22 kuikabili Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Azam Complex.

 

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!