CHIRWA AMKIMBIZA STRAIKA AZAM
Ujio wa Obrey Chirwa umesababisha Ditram Nchimbi aondolewe katika kikosi cha Azam.
Nchimbi alikuwa tegemeo kwenye kikosi cha Njombe Mji iliyoshuka daraja msimu uliiopita wa Ligi Kuu Bara kabla ya kusajiliwa na Azam, lakini ameshindwa kuonyesha kiwango kilichotarajiwa akiwa Azam.
Kutua kwa Chirwa kumeongeza idadi ya washambuliaji kufikia sita, wengine wakiwa ni Donald Ngoma, Mbaraka Yusuph, Danny Lyanga, Yahya Zayd na Tafazwa Kutinyu, hiyo ni baada ya kuondolewa Nchimbi.
Meneja wa timu hiyo, Philipo Alando alisema kuwa wamemtoa kwa mkopo Nchimbi kwenda ili akapate nafasi ya kucheza
WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam
Comments
Post a Comment