Posts

Showing posts from November, 2018

SIMBA WAWALAZA MBABANE SWALLOWS BAO 4-1

Image
Kikosi cha Simba kimefanikiwa kuanza vizuri leo katika mchezo wa Fainali za Mabingwa ya Afrika uliochezwa Uwanja wa Taifa kwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Mbabane Swallows FC ya Swaziland. Mabao ya Simba yalifungwa na John Bocco dakika ya 7 akimalizia pasi ya Nicolus Gyan kisha akafunga bao la pili dakika ya 32 kwa mkwaju wa penati baada ya Emmanuel Okwi kuchezewa rafu na mlinda mlango wa Mbabane. Mbabane waliweza kutikisa nyavu za Simba dakika ya 24 lililofungwa na Guevane Nzambe na kufanya kipindi cha pili kumalizika kwa bao 2-1. Simba walirejea kwa kasi kipindi cha pili na kufanikiwa kufanya mashambulizi na wakafunga bao la 3 lililofungwa na Meddie Kagere dakika ya 83 baada ya mlinda mlango wa Mbabane kuteleza akiwa na mpira kisha dakika ya 90 Clatous Chama alifunga bao la 4 akimalizia pasi ya Hassan Dilunga. Simba watatakiwa wasiruhusu bao wakienda ugenini ili waweze kusonga mbele katika hatua ya michuano hii kwa kuwa Mbabane sio timu ya kubeza

FEDHA ZA YONDANI ZAZUIA USAJILI YANGA SC

Image
KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ameuambia uongozi wa timu hiyo kuwa hawezi kufanya usajili wa wachezaji wapya kwenye dirisha dogo kwa kuwa wachezaji wake wengi bado wanadai fedha zao za usajili. Zahera mwenye uraia wa DR Congo na Ufaransa ameyasema hayo kufuatia beki wake wa kati, Kelvin Yondani na kipa Beno Kakolanya kugomea kujiunga na timu kufuatia kudai fedha kwenye timu hiyo. Yondani na Kakolanya wamegomea kujiunga na timu wakitokea kwenye kambi ya timu ya taifa, Taifa Stars kuelekea kwenye mechi mbili za Kanda ya Ziwa ambazo zote Yanga ilifanikiwa kushinda. Akizungumza na Championi Jumatano, Zahera alisema kuwa hawezi kufanya usajili wa wachezaji wapya katika usajili wa dirisha dogo iwapo viongozi wa timu hiyo watashindwa kumaliza matatizo ya wachezaji waliopo kwa sasa kwenye kikosi chake. “Kama ukimya basi fahamu kuna tatizo, unajua usajili ni kitu kikubwa, unaweza nyumbani kukawa na matatizo, mtoto wako haendi shule sasa sijui kama unaweza tena kuleta mtoto...

MAKAMBO AMFUNIKA VIBAYA KAGERE

Image
shambuliaji wa Yanga raia wa DR Congo, Heritier Makambo. MAMBO ni moto! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya mshambuliaji wa Yanga raia wa DR Congo, Heritier Makambo kuandika rekodi ya pekee hivi karibuni katika michuano ya Ligi Kuu Bara. Makambo ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kwenye Ligi Kuu Bara kufunga mabao kwenye michezo miwili mfululizo ya mkoani na kuwazidi Emmanuel Okwi pamoja na Mnyarwanda, Meddie Kagere wa Simba. Mnyarwanda, Meddie Kagere wa Simba. Makambo alifunga kwenye mechi dhidi ya Mwadui FC pamoja na Kagera Sugar ambazo zote Yanga walishinda. Ilianza dhidi ya Mwadui FC, Novemba 22, mwaka huu katika Uwanja wa Kambarage Shinyanga na katika mchezo huo Makambo aliifungia timu yake hiyo bao moja kati ya mabao ya mawili iliyoshinda. Baada ya hapo Yanga ilipambana na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba na katika mechi hiyo Makambo alifanikiwa kuifungia timu hiyo kwa mara nyingine bao moja kati ya mabao mawili ambayo iliyapata kwen...

MKUDE, CHAMA WAPEWA KAZI MAALUM KUIUA MBABANE

Image
SIMBA ipo ka­tika maandalizi makali ya mechi yake ya Juma­tano ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mbabane Swal­lows kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, kocha Mbel­giji, Patrick Aussems amewapa kazi maalumu viungo wake wawili,  Jo­nas Mkude na Mzambia, Cletus Chama. Akuzungumza na  Cham­pioni Jumatatu,  Mkude alisema kuwa Aussems amefikia hatua hiyo baada ya kukamilisha uchunguzi wake dhidi ya Mbabane Swallows.Alisema katika uchunguzi huo alibaini kuwa Mbabane wapo vizuri sehemu ya kiungo, ndiyo maana akaamua kuwapatia kazi maalumu. “Kwa sasa tunaendelea kujifua vilivyo ili tuweze kuwa fiti tayari kwa kuifanya kazi hiyo am­bayo kocha ametupatia, ni matumaini yangu kuwa ha­tutamwan­gusha kocha, tutaifan­ya kama anavyotaka. “ Kazi yenyewe hiyo kwa sasa si­wezi kuisema ila kwa yeyote atakayekuja uwanjani siku hiyo ataiona,” alisema Mkude ambaye hucheza nafasi ya kiungo mkabaji akishirikiana vilivyo na Mghana, James Kotei. Kwa upande wake Cha­ma yeye hucheza nafasi ya kiung...

CHIRWA AMKIMBIZA STRAIKA AZAM

Image
U jio wa Obrey Chirwa umesababi­sha Ditram Nchimbi aondolewe katika kikosi cha Azam. Nchimbi alikuwa tegemeo kwenye kikosi cha Njombe Mji iliyoshuka daraja msimu uliiopita wa Ligi Kuu Bara kabla ya kusajiliwa na Azam, lakini ameshindwa kuonyesha kiwango kilichotarajiwa akiwa Azam. Kutua kwa Chirwa kumeongeza idadi ya washambuliaji kufikia sita, wengine wakiwa ni Donald Ngoma, Mbaraka Yusuph, Danny Lyanga, Yahya Zayd na Tafazwa Kutinyu, hiyo ni baa­da ya kuondolewa Nchimbi. Meneja wa timu hiyo, Philipo Alando alisema kuwa wam­emtoa kwa mkopo Nchimbi kwenda ili akapate nafasi ya kucheza WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

KAPOMBE APASULIWA MGUU SAUZ

Image
B EKI wa kulia wa Sim­ba, Shomari Kapombe, amefanyiwa upasuaji wa mguu kufuatia kuu­mia enka kwenye kambi yaT­aifa Stars nchini Afrika Kusini. Beki huyo alikuwa kwenye kambi ya timu hiyo iliyokuwa ina­jiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu Afcon dhidi ya Lesotho katika mchezo uliopigwa nchini Lesotho, wikiendi iliopita. Beki huyo ambaye alilazimika kubakia nchini humo kwa ajili ya kupatiwa matibabu, juzi alifanyi­wa upasuaji wa mguu wake katika hospitali moja kubwa kwenye Jiji la Pretoria, Afrika Kusini. Akizungumza na  Championi Jumatatu,  mwenyekiti wa timu hiyo, Swedy Mkwabi alisema up­asuaji huo utamlazimu Kapombe kukaa nje ya uwanja kwa wiki sita. “Kesho Jumatatu (leo) atak­wenda tena hospitali kuonana na daktari wake ili kuangalia maen­deleo baada ya upasuaji kwa sababu atakuwa nje kwa muda wa wiki sita isipokuwa atarejea nchini wakati wowote kulingana na dak­tari wake atakavyokuwa ameon­gea naye,” alisema Mkwabi. WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

MBELGIJI SIMBA: NIMEPEWA JINA LA ULIMWENGU

Image
KOCHA  wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems ameweka wazi kuwa amekabidhiwa jina la mshambuliaji Thomas Ulimwengu. Ulimwengu ambaye amevunja mkataba wake na Al Hilal ya Sudan anatajwa kutakiwa na Simba kwa ajili ya kumtumia kwenye michuano ya kimataifa. Mshambuliaji huyo alikuwa na Taifa Stars nchini Lesotho katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa Afrika lakini hakuweza kucheza kutokana na kocha mkuu wa timu hiyo, Mnigeria, Emmanuel Amunike kumuweka benchi. Ulimwengu amecheza mechi mbili tu chini ya Amunike ambazo zilikuwa ni dhidi ya Uganda na ile mechi ya kwanza ya Cape Verde, hivyo Mbelgiji alitegemea amuone akicheza na Lesotho lakini haikuwa hivyo. Awali chanzo makini kutoka ndani ya Simba, kililiambia  Championi Jumamosi  kuwa, klabu hiyo ilikuwa kwenye mchakato wa kutaka kumsaini lakini kwa sasa inaonekana kama unaelekea kukwama kutokana na kocha kutomuona Ulimwengu akicheza licha ya kuambiwa ni mchezaji mzuri. “Usajili wa Ulimwengu bado ...

YANGA YATEKETEZA MAMILIONI MWANZA

Image
YANGA  imeendelea kuonyesha jeuri ya fedha, ni baada ya jana kutumia usafiri wa ndege kuwafuata wapinzani wao Kagera Sugar mkoani Kagera na ikiwa Mwanza kwa siku moja tu wametumia zaidi ya Sh milioni tatu. Yanga ilifika Mwanza Jumanne ambapo walipata msosi na siku hiyohiyo waliondoka jijini hapo kwa basi la kukodi kwenda Shinyanga kuwavaa Mwadui FC kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga. Baada ya kucheza mechi Alhamisi na kupata ushindi wa mabao 2-1, siku hiyohiyo usiku walirejea tena Mwanza wakiwa na basi la kukodi ambapo walikwenda kufikia kwenye hoteli kubwa ya The Pigeon ambapo walilala. Asubuhi yake wachezaji na benchi la ufundi walipata chakula na huduma zingine ambapo mpaka wanaondoka jana asubuhi kwenda mkoani Kagera, huku nyuma walikuwa wameteketeza zaidi ya milioni tatu. Hata hivyo pamoja na klabu hiyo kukumbwa na ukata, waliamua kutumia usafiri wa ndege ya Bombadier kutoka Mwanza hadi Kagera kwa ajili ya mechi ya kesho Jumapili ya ligi kuu dhidi ya Ka...

AMUNIKE KAA MGUU SAWA, SISI WATANZANIA NI WABRAZILI

Image
M WAKA  2001, timu ya taifa ya Brazil ilikuwa kwenye hatikati ya kuko­sa michuano ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza kutokana na mwenendo wa kusuasua wa timu hiyo. Inajulikana wazi kati ya nchi yenye presha kubwa ka­tika mchezo wa soka kuliko zote ni  Brazil , kuna sababu kubwa kama tatu hivi, kwan­za ni vipaji vingi walivyona­vyo, pili ni wingi wa watu wa taifa hilo (inakaridiwa wapo zaidi ya watu milioni 200) na tatu ni kuwa kila mtu ni kocha kwenye taifa hilo. Kuna wakati ilifika hatua un­aweza kupanga vikosi vitano vya taifa la Brazil na vyote vikawa bora na vinaweza ku­fika fainali ya Kombe la Dunia. Juni 2001, Luiz Felipe Scolari aliteuliwa kuwa ko­cha wa taifa hilo, presha ili­kuwa kubwa, alianza mch­ezo wa kwanza vibaya kwa kufungwa na Uruguay bao 1-0, baada ya hapo akaen­delea vizuri na mwisho aka­tangaza kumuacha kikosini ‘Mungu’ wa soka wa wakati huo kwa Wabrazili, Romário. Ilikuwa ngumu kwa Wa­brazili kumuelewa kwa kuwa waliamini Romario ndi...

MADRID WAMFUATA RASHFORD ENGLAND

Image
K LABU  ya Real Madrid im­eonekana kuweka nguvu yake kwenye usajili kwa sasa baada ya kutenga kitita cha pauni milioni 90 (zaidi ya shilingi bilioni 200), kwa ajili ya kumsa­jili Marcus Rashford wa Man United na Christian Eriksen wa Tottenham Hotspur. Madrid hawapo kwenye kiwango kizuri zaidi kwa sasa na wanatakiwa kuhakikisha wanafanya usajili kabambe ili kujiwek a kwenye mazingira mazuri ya kutwaa makombe msimu huu. Mabosi wa Real Madrid walikuwa uwanjani kumtazama mshambuliaji Rashford wakati akiichezea England ilipokuwa ikivaana na Croatia kwenye Dimba la Wembley. Madrid wanaamini kuwa mshambuliaji huyu anaweza kuziba pengo la Cristiano Ronaldo ambaye aliondoka kwenye timu hiyo na kujiunga na Juventus. Madrid ambao ndiyo mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya pia wanamtaka kiungo wa Spurs, Eriksen kwa ajili ya kuziba pengo la Luka Modric ambaye wanaamini kuwa mwishoni mwa msimu huu anaweza kuondoka kwenye timu hiyo. Kocha wa United, Jose Mourinho ameonek...

MASTAA 5 WALIOTWAA TAJI LA LIGI YA UEFA WAKIWA NA TIMU 2 AU ZAIDI

Image
KILELE cha sifa katika soka la klabu barani Ulaya ni kushiriki na kutwaa taji la  Ligi ya Ubingwa ya UEFA (UCL).  Makocha na wachezaji wengi hulichukulia taji la ligi hiyo kuwa linashika nafasi ya pili duniani kwa heshima baada ya Kombe la Dunia. Baadhi ya wanasoka wakubwa duniani wameshinda mataji ya UCL ambao ni pamoja na  Ronaldo na Gianluigi Buffon. Wengine ni Messi, Andries Iniesta, Iker Casillas na Paulo Maldini ambao wamelitwaa japo kwa klabu moja tu.  Wafuatao ni wachezaji watano walioshinda taji hilo wakiwa na klabu zaidi ya moja. .  Clarence Seedorf  : Mholanzi huyo alishinda kombe hilo mara ya kwanza akiwa na klabu ya Ajax Amsterdam msimu wa 1994/1995, akalitwaa tena akiwa na Real Madrid mnamo 1997/1998. Mara ya tatu alishinda akiwa na AC Milan mnamo 2002. Kiungo huyo aliisaidia Milan mara mbili, mnamo 2003/ 2004 na 2006/ 2007. 2.  Samuel Eto’o,    mshambuliaji wa  Cameroon, alikuwa ni mmoja wa washam...

MAN U YATAYARISHA BN. 77 KUMCHUKUA PELLEGRINE WA ROMA

Image
Lorenzo Pellegrini Manchester United ya Uingereza wanatayarisha kitita cha Pauni Bil. 26 kumchukua kiungo wa timu ya Roma ya Italia, Lorenzo Pellegrini, mwezi Januari mwaka ujao huku timu yake hiyo ikitia ngumu kutomwachia kirahisi. Kocha Jose Mourinho wa Man U ambaye ni kipenzi mkubwa wa soka la Pellegrini (22) anayechezea pia  timu ya taifa ya Italia, anataka kumnasa na kumwongeza mshahara wake wa Paundi 890,000 kwa mwaka, kuwa mara mbili; yaani ufikie Sh. bil. 6.7. Gazeti la michezo la  Italia la  Corriere dello Sport s, limesema wakala wa Pellegrini aitwaye Giacomo Pocetta, alikutana na wakurugenzi wa United jijini Londoni  ambako klabu hiyo ilipendekeza donge hilo nono.

KAPOMBE KUBAKIA SAUZ

Image
B EKI  wa kulia wa Simba, Shomari Kapombe, atalazimika kubakia Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu kufuatia majeraha ya kuvunjika mguu aliyoyapata akiwa na timu ya taifa, Taifa Stars nchini Afrika Kusini. Kapombe aliumia akiwa kwenye kambi ya timu hiyo iliyokuwa inajiandaa na mchezo wa kufuzu Afcon uliopigwa kwenye Uwanja wa Setsoto hapa Maseru, Lesotho, jana Jumapili. Taarifa ambazo  Championi Jumatatu  limezipata kutoka kwa viongozi wa Simba, zinasema kuwa beki huyo atalazimika kubakia Afrika Kusini kwa ajili ya kupatiwa matibabu kwa daktari wake maalum kabla ya kurejea nchini kuendelea na majukumu ya timu yake. Awali kabla ya kufikia makubaliano juu ya mchezaji huyo kubakia nchini humo, uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ulipanga kumpeleka Dubai kwa ajili ya kupata matibabu hayo lakini viongozi wa Simba waliopo nchini hapa wamependekeza abakie Afrika Kusini kwa kuwa ana daktari wake maalum. Beki huyo amevunjika mguu karibu na eneo la enka ...

AFTER PIGEON LESOTHO, NATIONAL STARS RETURN TO THE WORLD

Image
Tanzania National Team #TaifaStars has arrived in the evening on Monday, November 19, 2018 from Lesotho on the African Football Championship qualifying match in AFCON2019Q which ended in Tanzania for 1-0 in Lesotho.

Majembe manne kumrithi Okwi

Image
KADI mbili za njano alizopata straika Emmanuel Okwi, zimewanyima usingizi Waganda kuelekea mchezo wao wa kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ya Afcon dhidi ya Cape Verde na sasa benchi lao la ufundi linaumiza kichwa kujua nani atakuwa mbadala wake. Okwi ambaye kwa sasa ni kama roho ya timu hiyo ya Taifa ya Uganda kutokana na kufunga mabao muhimu, ataukosa mchezo huo utakaochezwa Jumamosi ya wiki hii Uwanja wa Namboole, nchini humo. DIMBA Jumatano liliwasiliana na mwandishi wa habari nguli kutoka nchini Uganda, David Isabirye, ambaye alisema kutokuwepo kwa Okwi kunawafanya wachezaji wanne kuandaliwa ili mmoja avae viatu vyake. “Ni kweli Okwi hatakuwepo mchezo huo dhidi ya Cape Verde wa Jumamosi inayokuja kutokana na kutumikia adhabu ya kadi mbili za njano, anaweza akacheza leo (jana) mchezo wa kirafiki dhidi ya Nigeria tu,” alisema. Alisema mmoja wa wachezaji hao anayeweza angalau kuziba pengo la Okwi, ni Milton Karisa anayechezea Klabu ya Mouloudia Club D’Oujda ya nchini Moro...

Simba ya MO ni balaa tupu

Image
IN SUMMARY Katika mechi zao 11 walizocheza mpaka sasa, Simba imevuna jumla ya mabao 23 ikiwa ndiyo klabu yenye mabao mengi zaidi kuliko nyingine zinazoshiriki ligi hiyo kwa msimu huu yenye timu 20. ADVERTISEMENT ADVERTISEMENT MASHABIKI wa Simba kwa sasa wana kila sababu ya kunenepa. Wakonde wana stresi gani bwana, wakati mkwanja wa bilionea wao, Mohammed ‘MO’ Dewji unaendelea kuwapa raha duniani kutokana na timu yao kukimbiza Bongo. Ikiwa katika mbio za kutetea taji lao la Ligi Kuu Bara walilolitwaa msimu uliopita baada ya kulisotea kwa miaka mitano, Simba ya sasa ni moto ikiwakimbiza wapinzani wao, ikiwamo Yanga iliyowatesa kwa miaka kadhaa walipokuwa ovyo. Kama hujui ni kwamba safu ya ushambuliaji ya Simba kwa sasa inathibitisha jeuri ya fedha ya timu yao kulingana na watani zao wa Yanga ambao, wanaishi maisha ya kuungaunga kwa sasa kutokana na hali yao ya uchumi kuyumba. Kiwango kikubwa cha fedha ambacho Simba imekuwa ikitumia kulipa mishahara nyota ...

Manchester Dabi: Wako wapi Mashetani Wekundu tuliowazoea?

Image
IN SUMMARY Kwa mujibu wa rekodi, Manchester United wanaongoza kwa ubabe, ambapo katika michezo 176 ya Dabi iliyopigwa huko nyuma, Mashetani wekundu walishinda mara 73 na City wameshinda mechi 51 huku michezo 52, zikimalizika kwa sare. ADVERTISEMENT ADVERTISEMENT Manchester, England. Leo Usiku, majira ya saa 1:30, saa za Afrika Mashariki, macho na masikio yataelekezwa katika Jiji la Manchester. Shughuli zote zitasitishwa. Maduka yatafungwa. Safari hii shoo ya kibabe inapigwa pale Etihad. Manchester City, wanawaalika mahasimu wao, Manchester United. Patachimbika leo! Naam, kipute cha mahasimu ndio kimewadia mwanangu. Mwamuzi ameshajulikana. Sio mwengine bali ni mtoto wa nyumbani, uzao wa Jiji la Manchester, Anthony Taylor. Hii ndio mechi yake ya kwanza ya Manchester Dabi. Ila hiyo sio ishu. Ikiwa ni Dabi ya 177, ulimwengu utamshuhudia, Jose Mourinho akiliongoza jeshi lake kumfuata hasimu wake mkubwa Pep Guardiola kwenye dimba la Etihad kuwania kusaka kama sio pointi t...

Okwi, Kagere waibeba Simba kwa Yanga msimamo Ligi Kuu

Image
IN SUMMARY Sare ya bao 1-1, iliyopata Yanga dhidi ya Ndanda Jumapili iliyopita ndiyo iliyowapa kicheko Simba na kuendelea kusalia katika nafasi ya pili kwenye msimamo. ADVERTISEMENT ADVERTISEMENT Dar es Salaam. Licha ya Simba na Yanga zote kuwa na pointi 26,safu ya ushambuliaji ya wekundu wa Msimbazi inayoongozwa na Emmanuel Okwi na Meddy Kagere imeonekana kuibeba timu hiyo kwenye msimamo wa ligi. Mabao 23 iliyofunga Simba mpaka sasa kwenye ligi yamewawezesha kuendelea kuishikilia nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi na kuwa juu ya watani zao Yanga walio nafasi ya tatu licha ya timu hizo zote mbili kuwa sawa kwa pointi 26. Okwi na Kagere peke yao wamefunga mabao 14 wakizidiwa mawili na timu nzima ya Yanga ambayo imefunga mabao 16. Hata hivyo sare ya bao 1-1 iliyopata Yanga dhidi ya Ndanda Jumapili iliyopita ndiyo iliyowapa kicheko Simba na kuendelea kusalia katika nafasi ya pili kwenye msimamo. Kama Yanga ingeshinda siku hiyo basi Simba ingeshuka ...