SUAREZ AAGA BARCELONA



Denis Suarez
WINGA Denis Suarez aliiaga vizuri Barcelona baada ya kucheza vizuri kwenye mechi ya Copa del Rey, Alhamisi iliyopita.
Suarez anatazamiwa kuondoka katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili na kujiunga na Arsenal.
Arsenal inataka kumchukua kwa mkopo Suarez ili kuongeza makali ya safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.

Kocha wa Arsenal, Unai Emery ndio anamtaka Suarez kwani aliwahi kufanya naye kazi akiwa Sevilla.
Pamoja na kuwa Barcelona ililala mabao 2-1 kwenye mechi dhidi ya Levante, Suarez ndio alisababisha penalti iliyosaidia Barcelona kupata bao litalowasaidia kwenye mechi ya marudiano.

Philippe Coutinho ndio alifunga penalti ya Barcelona kwenye mechi hiyo iliyopigwa katika Uwanja wa Ciudad de Valencia.
Suarez alijituma kwenye mchezo huo kwani alikuwa ndio chachu ya mashambulizi ya timu hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!