MWANA FA: HATA WAJE BARCELONA KWA SIMBA HII HAWATOKI
MKALI wa michano Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’, ameungana na msemaji wa Wekundu wa Msimbazi, Haji Manara, kusema kwamba hata Barcelona wakija Dar kwa Simba hii wanaacha pointi tatu.
MwanaFA ambaye ni shabiki wa kutupwa wa Simba, amefikia kutoa kauli hiyo baada ya juzi timu yake kuichabanga JS Saoura ya Algeria kwa mabao 3-0 kwenye mchezo wa kwanza wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika.
Lakini kabla ya mchezo huo, Manara alisema kuwa kwa Simba hii, hata wangepangwa na Bayern Munich ya enzi zile, Barcelona ya akina Xavi na Manchester City, lazima washinde Uwanja wa Taifa.
Akizungumza na Championi Jumatatu FA alisema kwenye kundi lao hakuna timu itakayoisumbua Simba kwa sababu kikosi chao kimeimarika mara tano ya kilivyokuwa awali, hivyo levo yao kwa sasa ni kucheza dhidi ya Barcelona au Bayern na siyo vitimu vidogo kama JS Saoura.
“Wale walikuwa wanakufa saba na siyo tatu, we si umeona Pascal Wawa alichokuwa anakifanya, ulimuona James Kotei? Kwa hiyo ile ndiyo Simba.
“Sasa hivi inatakiwa tupangiwe na Barcelona na Bayern Munich na siyo vitimu hivi vya ajabuajabu, ni kutuvunjia heshima,” alisema FA.
Comments
Post a Comment