SIMBA KUSHUSHA MZIKI MNENE PEMBA
KAMA Azam walijua kwamba Simba itachezesha kikosi B kwenye fainali za Mapinduzi wamechemka. Simba inashusha mziki wote leo mjini Pemba.
Katika mchezo huo Simba na Azam zitakuwa zinakutana kwa mara ya tatu fainali kwenye michuano hiyo ambapo mara ya kwanza zilikutana fainali mwaka 2012, 2017 na sasa 2019.
Azam Fc ndiyo mabingwa watetezi wa kombe hilo wametwaa mara mbili mfululizo sasa.
Meneja wa Simba, Abbas Ali alisema kuwa; “Baadhi ya wachezaji watatakiwa kwenda kuungana na wenzao kule Pemba na hii ni kutokana na kocha jinsi atakavyokuwa amepanga nani aende na nani abaki na lengo ni kupata matokeo.”
Mudhathir Yahya wa Azam Fc, amesisitiza kuwa watapamba katika fainali dhidi ya Simba leo kwani anajua kwamba watapania na wakishinda watatamba sana.
Yussuf Mlipili wa Simba alisema hawatowaangalia usoni Azam katika fainali ya leo kwani wanataka kuthibitisha kwamba wao ni imara na wana kikosi kipana.
Comments
Post a Comment