MZUNGU ASHANGAA NIYONZIMA KUKAA.. BENCHI SIMBA
KOCHA wa Azam FC, Mholanzi Hans van Der Pluijm amefunguka kuwa kiwango ambacho Simba ilionyesha dhidi ya Waarabu kilikuwa bora ingawa anashangaa kwa nini Haruna Niyonzima amekuwa hatumiki licha ya kuwa na kiwango bora.
Pluijm alisema Simba imekuwa katika kiwango bora katika mechi za kimataifa kutokana na kila idara kuonekana kukamilika ndiyo maana wamekuwa wakitoa vipigo.
Wikiendi iliyopita Simba ilifanikiwa kushinda kwa mabao 3-0 dhidi ya JS Saoura ya Algeria katika mechi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika lakini kesho yake ilichapwa mabao 2-1 na Azam FC kwenye fainali ya Kombe la Mapinduzi.
Hans alisema kiwango ambacho ameonyesha Niyonzima katika Mapinduzi kilikuwa bora japo vijana wake walikuwa bora zaidi na kuweza kutwaa ubingwa.
“Simba inafanya vizuri kimataifa hilo halina ubishi timu imekamilika katika kila idara hilo halina ubishi, mchezaji kama Niyonzima kiwango chake kwa sasa kimekuwa bora nimeona katika Mapinduzi japo sijui kwa nini amekuwa hatumiki mara kwa mara ingawa sisi makocha kila mmoja huwa na falsafa zake na maamuzi hivyo siwezi muingilia kocha katika hilo.
“Na kitendo cha Simba kuifunga JS Saoura siyo kazi ndogo zaidi ni wao kuendelea kupambana katika mechi zijazo, ninaamini kuwa watafanya vyema hata kwa hao AS Vita,” alisema Pluijm.
Comments
Post a Comment