SIMBA TISHIO CAF, WAIGONGA JS SAOURA BAO 3-0
TIMU ya Simba wamefanikiwa kuwapa furaha mashabiki wao na Watanzania kwa Ujumla baada ya kuibuka na ushindi wa bao 3-0 dhidi ya timu ya Jeunesse Sportive de la Saoura maarufu kama ‘JS Saouro’ kutoka nchini Algeria.
Mchezo huo wa Kundi D wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika, umepigwa leo Jumamosi, Januari 12, katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji Emmanuel Okwi ndiye alikuwa wa kwanza kuiandikia Simba bao la kuongoza dakika ya 45+2 kabla ya kwenda mapumziko baada ya kufanya shambulizi hatari na kuwahesabu mabeki wa JS Saoura.
Simba waliokuwa wakishambulia muda wote wa mchezo huo, Meddie Kagere alifanikiwa kuiandikia Simba bao la pili 51 kisha kurudi tena nyavuni dakika 16 baadaye na kuiandikia tena bao la tatu dakika ya 67.
Mpaka dakika 90 zinakwisha, Simba wamefanikiwa kuondoka na pointi tatu muhimu kwa kuwapiga Waarabu hao bao 3-0.
Mechi nyingine za leo za CAF
FC Platinum 0- 0 Orlando Pirates
TP Mazembe 2 – 0 Ismaily SC
PICHA: MUSA MATEJA, SWEETBERT LUKONGE NA RICHARD BUKOS, GPL
Comments
Post a Comment