MORATA ANUKIA ATLETICO MADRID



Alvaro Morata
KUNA taarifa kuwa Chelsea ipo tayari kumruhusu Alvaro Morata kujiunga na Atletico Madrid.
Habari zaidi zinaeleza kuwa Morata anafukuziwa pia na timu za Bayern Munich, Borussia Dortmund, PSG na Roma.
Watu walio karibu na Morata wanadai kuwa staa huyo hana furaha katika timu ya Chelsea.

Hali hiyo imechangiwa kutokana na ukame wa mabao unaomkabili kiasi cha kuanza kufikiria pengine aondoke Chelsea.
Hata hivyo, uwezekano mkubwa wa Morata kuondoka itakuwa kwa njia ya mkopo kutokana na kupokea mshahara mkubwa kutoka Chelsea.

Hata hivyo, habari zaidi zinaeleza kuwa Chelsea wapo tayari kumuuza hata kwa bei ya hasara na wamewasiliana na Atletico.

Morata amepachika mabao matano katika mechi 16 za Ligi Kuu England alizocheza msimu huu.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!