KISA SIMBA, WAARABU WAVUTA JEMBE LINGINE
BAADA ya kumsainisha mshambuliaji Mtanzania, Thomas Ulimwengu, Klabu ya JS Saoura ya Algeria, imevuta jembe lingine tayari kwa kuwakabili Simba Jumamosi ijayo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. JS Saoura itapambana na Simba kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi wa michuano hiyo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Kundi D pia lina timu za Al Ahly ya Misri na AS Vita ya DR Congo. Sasa kwa mujibu wa taarifa kutoka Algeria ni kwamba JS Saoura imemsajili mshambuliaji, Rafik Boukbouka aliyetokea Klabu ya Us Beni Douala ya Algeria ambayo ipo ligi ya madaraja ya chini kwa mkataba wa miaka mitatu.
Saoura imemsajili Boukbouka baada ya kuvutiwa na kasi yake ya utupiaji mabao ambapo mpaka anaondoka Us Beni Douala, alikuwa Ibrahim Mussa, Dar es Salaam BAADA ya kumsainisha mshambuliaji Mtanzania, Thomas Ulimwengu, Klabu ya JS Saoura ya Algeria, imevuta jembe lingine tayari kwa kuwakabili Simba Jumamosi ijayo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
JS Saoura itapambana na Simba kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi wa michuano hiyo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Kundi D pia lina timu za Al Ahly ya Misri na AS Vita ya DR Congo. Sasa kwa mujibu wa taarifa kutoka Algeria ni kwamba JS Saoura imemsajili mshambuliaji, Rafik Boukbouka aliyetokea Klabu ya Us Beni Douala ya Algeria ambayo ipo ligi ya madaraja ya chini kwa amefunga mabao 16 kitu ambacho timu hiyo inaamini itaongeza kitu kwenye safu yao ya ushambuliaji.
Huu ni usajili wa pili baada ya awali kumsaini Ulimwengu aliyetokea Al Hilal ya Sudan kama mchezaji huru. Kutokana na usajili huo, timu hiyo inaonekana kujiimarisha zaidi kwenye safu yao ya ushambuliaji.
Comments
Post a Comment