‘MO SALAH ANAPOTEZA MUDA LIVER’

Mo Salah amekuwa katika kiwango kizuri kwa misimu miwili, msimu huu ameifanya timu yake iwe moja ya zinazowania ubingwa katika Premier League. Hadi sasa Salah, 26, amefunga mabao 16 katika michezo
27 ya michuano yote akiiongoza Liverpool kuongoza kwenye msimamo wa Premier pamoja na kufuzu hatua ya mtoano katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
27 ya michuano yote akiiongoza Liverpool kuongoza kwenye msimamo wa Premier pamoja na kufuzu hatua ya mtoano katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Akizungumzia uwezo wa raia mwenzake huyo wa Misri, Mido, 35, alisema: “Huwezi kujua litakalotokea kwenye soka. Barcelona au Real Madrid zikikutaka lazima kichwa kichemke, mchezaji yeyote yupo hivyo.” Akaongeza kuwa ikiwa msimu huu pia atafikisha mabao 25 anaamini vigogo hao watamfuata kwa nia ya kumsajili.
“Nafikiri wanasubiri kuona msimu huu atafanya nini, hawawasajili wachezaji wanaong’ara kwa msimu mmoja tu. Akifikia malengo wanayotaka, litakuwa jambo gumu kumzuia, huo ndiyo ukweli,” alisema.
Comments
Post a Comment