Posts

Showing posts from January, 2019

NUNUA GAZETI LA CHAMPIONI UJISHINDIE SIMU NA MKWANJA

Image
anuary 16, 2019 by  Global Publishers GAZETI la Championi kuanzia leo litakuwa na zawadi mbalimbali kwa ajili ya wasomaji wake. Msomaji atakayenunua gazeti hili na mengine ya Championi atakuwa na nafasi ya kujishindia fedha taslimu kuanzia shilingi 5000, 10,000, 20,000, simu za mkononi na zawadi nyingine nyingi. Unachotakiwa kufanya ni kununu gazeti, fungua ndani kwenye ukurasa mmoja utakuta stika ambayo imebandikwa, ifungue utakuta zawadi yako ndani, baada ya hapo piga simu kwenye namba iliyopo kwenye stika hiyo na ujitambulishe jina, umri, sehemu ulipo na zawadi uliyoshinda. Baada ya hapo utapewa maelekezo ya jinsi ya kupata zawadi yako. Angalizo usipoteze gazeti wala kuponi ulioshindia zawadi hiyo, kadiri unavyonunua magazeti mengi ndiyo una nafasi ya kushinda zawadi nyingi zaidi. Na Mwandishi Wetu

JOELLE BUKURU… MRUNDI WA SIMBA ANAYETAMANI KUICHEZEA TWIGA STARS

Image
LIGI ya Wanawake inazidi kuunguruma kwenye viwanja tofauti huku vipaji kibao vikishuhudiwa kutoka katika timu 12 zinazoshiriki ligi hiyo inayozaminiwa na kinywaji cha Serengeti Lite. Simba Queens ni miongoni mwa timu shiriki kunako ligi hiyo na tayari imeshashuka dimbani katika michezo mitano na kuvuna jumla ya pointi 13. Nyuma ya mafanikio hayo yupo mchezaji nyota wa Kikosi hicho, Joelle Bukuru ambaye anacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji. Mrundi huyo huu ni msimu wake wa kwanza ndani ya ligi hiyo akiwa na jezi ya Simba. Amekuja nchini na mwenzake anayeitwa Aisha Djafar. Joelle Bukuru (kushoto mwenye mpira) akifanya yake. Bukuru ni miongoni mwa nyota ambao Jumapili iliyopita waliisaidia Simba kuibuka na ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Yanga Princess katika mwendelezo wa ligi hiyo, mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Karume, Dar. Championi Jumatano  limefanya mahojiano na nyota huyo juu ya maisha yake ya kwa jumla. “Naitwa Joelle Bukuru, nimezaliwa Burundi kati...

MZUNGU ASHANGAA NIYONZIMA KUKAA.. BENCHI SIMBA

Image
Haruna Niyonzima. KOCHA wa Azam FC, Mholanzi Hans van Der Pluijm amefunguka kuwa kiwango ambacho Simba ilionyesha dhidi ya Waarabu kilikuwa bora ingawa anashangaa kwa nini Haruna Niyonzima amekuwa hatumiki licha ya kuwa na kiwango bora. Pluijm alisema Simba imekuwa katika kiwango bora katika mechi za kimataifa kutokana na kila idara kuonekana kukamilika ndiyo maana wamekuwa wakitoa vipigo. Wikiendi iliyopita Simba ilifanikiwa kushinda kwa mabao 3-0 dhidi ya JS Saoura ya Algeria katika mechi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika lakini kesho yake ilichapwa mabao 2-1 na Azam FC kwenye fainali ya Kombe la Mapinduzi. Hans alisema kiwango ambacho ameonyesha Niyonzima katika Mapinduzi kilikuwa bora japo vijana wake walikuwa bora zaidi na kuweza kutwaa ubingwa. “Simba inafanya vizuri kimataifa hilo halina ubishi timu imekamilika katika kila idara hilo halina ubishi, mchezaji kama Niyonzima kiwango chake kwa sasa kimekuwa bora nimeona katika Mapinduzi japo siju...

ZAHERA ATAJA ALIPO MAKAMBO

Image
Mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makambo raia wa DR Congo. BAADA ya mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makambo raia wa DR Congo kudaiwa kutoweka klabuni hapo huku taarifa zake zikiwa hazieleweki alipo, kocha wa kikosi hicho, Mwinyi Zahera amemuibua mshambuliaji huyo. Makambo mwenye mabao 11 akiwa kinara wa ufungaji kwenye Ligi Kuu Bara, inadaiwa aliondoka Yanga takribani wiki mbili zilizopita. Tangu aondoke nchini, mawasiliano yake na viongozi wa klabu hiyo hayakuwa mazuri hali ambayo ilizua maswali mengi. Heritier Makambo raia wa DR Congo. Mshambuliaji huyo ambaye jana Jumanne alikosekana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao timu yake ilicheza dhidi ya Mwadui FC katika Uwanja wa Taifa, Dar, anatarajiwa kuwepo katika mchezo ujao dhidi ya Stand United, mwishoni mwa wiki hii. Zahera raia wa DR Congo kama ilivyo kwa Makambo, kipa wa timu hiyo, Klaus Kindoki na kiungo, Papy Tshishimbi, ameliambia  Championi Jumatano  kuwa: “Makambo alienda DR Congo na anarudi Ju...

MWANA FA: HATA WAJE BARCELONA KWA SIMBA HII HAWATOKI

Image
M KALI  wa michano Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’, ameungana na msemaji wa Wekundu wa Msimbazi, Haji Manara, kusema kwamba hata Barcelona wakija Dar kwa Simba hii wanaacha pointi tatu. MwanaFA ambaye ni shabiki wa kutupwa wa Simba, amefikia kutoa kauli hiyo baada ya juzi timu yake kuichabanga JS Saoura ya Algeria kwa mabao 3-0 kwenye mchezo wa kwanza wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika. Lakini kabla ya mchezo huo, Manara alisema kuwa kwa Simba hii, hata wangepangwa na Bayern Munich ya enzi zile, Barcelona ya akina Xavi na Manchester City, lazima washinde Uwanja wa Taifa. Akizungumza na  Championi Jumatatu  FA alisema kwenye kundi lao hakuna timu itakayoisumbua Simba kwa sababu kikosi chao kimeimarika mara tano ya kilivyokuwa awali, hivyo levo yao kwa sasa ni kucheza dhidi ya Barcelona au Bayern na siyo vitimu vidogo kama JS Saoura. “Wale walikuwa wanakufa saba na siyo tatu, we si umeona Pascal Wawa alichokuwa anakifanya, ulimuona James Kotei? Kwa hiyo ile ndiyo...

MORATA ANUKIA ATLETICO MADRID

Image
Alvaro Morata KUNA taarifa kuwa Chelsea ipo tayari kumruhusu Alvaro Morata kujiunga na Atletico Madrid. Habari zaidi zinaeleza kuwa Morata anafukuziwa pia na timu za Bayern Munich, Borussia Dortmund, PSG na Roma. Watu walio karibu na Morata wanadai kuwa staa huyo hana furaha katika timu ya Chelsea. Hali hiyo imechangiwa kutokana na ukame wa mabao unaomkabili kiasi cha kuanza kufikiria pengine aondoke Chelsea. Hata hivyo, uwezekano mkubwa wa Morata kuondoka itakuwa kwa njia ya mkopo kutokana na kupokea mshahara mkubwa kutoka Chelsea. Hata hivyo, habari zaidi zinaeleza kuwa Chelsea wapo tayari kumuuza hata kwa bei ya hasara na wamewasiliana na Atletico. Morata amepachika mabao matano katika mechi 16 za Ligi Kuu England alizocheza msimu huu.

SUAREZ AAGA BARCELONA

Image
Denis Suarez WINGA Denis Suarez aliiaga vizuri Barcelona baada ya kucheza vizuri kwenye mechi ya Copa del Rey, Alhamisi iliyopita. Suarez anatazamiwa kuondoka katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili na kujiunga na Arsenal. Arsenal inataka kumchukua kwa mkopo Suarez ili kuongeza makali ya safu ya ushambuliaji ya timu hiyo. Kocha wa Arsenal, Unai Emery ndio anamtaka Suarez kwani aliwahi kufanya naye kazi akiwa Sevilla. Pamoja na kuwa Barcelona ililala mabao 2-1 kwenye mechi dhidi ya Levante, Suarez ndio alisababisha penalti iliyosaidia Barcelona kupata bao litalowasaidia kwenye mechi ya marudiano. Philippe Coutinho ndio alifunga penalti ya Barcelona kwenye mechi hiyo iliyopigwa katika Uwanja wa Ciudad de Valencia. Suarez alijituma kwenye mchezo huo kwani alikuwa ndio chachu ya mashambulizi ya timu hiyo.

SIMBA KUSHUSHA MZIKI MNENE PEMBA

Image
Wachezaji wa timu ya Simba SC KAMA Azam walijua kwamba Simba itachezesha kikosi B kwenye fainali za Mapinduzi wamechemka. Simba inashusha mziki wote leo mjini Pemba. Katika mchezo huo Simba na Azam zitakuwa zinakutana kwa mara ya tatu fainali kwenye michuano hiyo ambapo mara ya kwanza zilikutana fainali mwaka 2012, 2017 na sasa 2019. Azam Fc ndiyo mabingwa watetezi wa kombe hilo wametwaa mara mbili mfululizo sasa. Meneja wa Simba, Abbas Ali alisema kuwa; “Baadhi ya wachezaji watatakiwa kwenda kuungana na wenzao kule Pemba na hii ni kutokana na kocha jinsi atakavyokuwa amepanga nani aende na nani abaki na lengo ni kupata matokeo.” Mudhathir Yahya wa Azam Fc, amesisitiza kuwa watapamba katika fainali dhidi ya Simba leo kwani anajua kwamba watapania na wakishinda watatamba sana. Yussuf Mlipili wa Simba alisema hawatowaangalia usoni Azam katika fainali ya leo kwani wanataka kuthibitisha kwamba wao ni imara na wana kikosi kipana.

AZAM FC MABINGWA MARA TATU MFULULIZO KOMBE LA MAPINDUZI

Image
Timu ya Azam FC wameifunga Simba SC kwa bao 2-1 kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, na kufanikiwa kutwaa Kombe la Mapinduzi kwa Mara ya 3 sasa. Wafungaji wa Azam ni Mudathir Yahya na  Obrey Chirwa ameifungia Azam FC bao la pili akimalizia kwa kichwa krosi ya Nickolas Wadada dakika ya 72. Bao la Simba lililofungwa na Yusuph Mlipili dakika ya 63.

SPURS V MAN UNITED…VITA YA KIBABE KILA KONA

Image
Wachezaji wa Manchester United  MANCHESTER United na Tottenham Hotspur zinatazamiwa kuvaana leo Jumapili kwenye mechi kali ya Ligi Kuu England itakayopigwa kwenye Uwanja wa Wembley jijini London. Wachambuzi wa soka wanaamini kuwa mchezo huo ndio utakaopima uwezo wa kocha wa muda wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer. Solskjaer ameshinda mechi tano mfululizo tangu alipopewa nafasi hiyo ingawa wataalamu wa soka wanadai ilikuwa dhidi ya timu ndogo. Kitendo cha kukabiliana na Spurs kwenye Uwanja wa Wembley kitakuwa kipimo kikubwa cha Mnorway huyo. Solskjaer anafahamu fika kuwa akishinda mchezo huu atakuwa ametengeneza mazingira mazuri ya timu yake kutinga kwenye nne bora ya Ligi Kuu England na kupata tiketi ya kucheza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Kama mchezo huu ungechezwa mwezi mmoja nyuma, timu ya Pochettino ingepewa nafasi kubwa ya kushinda kutokana na jinsi Manchester United ilivyokuwa inacheza soka mbovu chini ya kocha wa zamani, Jose Mourinho. ...

SIMBA TISHIO CAF, WAIGONGA JS SAOURA BAO 3-0

Image
Kikosi cha timu ya Simba kilichoanza dhidi ya JS Saoura TIMU ya  Simba  wamefanikiwa kuwapa furaha mashabiki wao na  Watanzania  kwa Ujumla baada ya kuibuka na ushindi wa bao 3-0 dhidi ya timu ya  Jeunesse Sportive de la Saoura  maarufu kama  ‘JS Saouro’  kutoka nchini  Algeria. Kikosi cha JS Saoura kilichoanza dhidi ya Simba. Mchezo huo wa  Kundi D  wa  Ligi ya Mabingwa  barani  Afrika , umepigwa leo Jumamosi, Januari 12, katika Uwanja wa Taifa jijini  Dar es Salaam. Mshambuliaji Emmanuel Okwi ndiye alikuwa wa kwanza kuiandikia Simba bao la kuongoza dakika ya 45+2 kabla ya kwenda mapumziko baada ya kufanya shambulizi hatari na kuwahesabu mabeki wa JS Saoura. Simba waliokuwa wakishambulia muda wote wa mchezo huo, Meddie Kagere alifanikiwa kuiandikia Simba bao la pili 51 kisha kurudi tena nyavuni dakika 16 baadaye na kuiandikia tena bao la tatu dakika ya 67. Mpaka dakika 90 zinakwisha, Si...