Posts

Showing posts from 2018

CHUKUA MKOPO WA HARAKA NA UPEWE BONUS YA TSH.10,000/= KWA M-PESA AU TIGOPESA KUPITIA "BRANCH".

Image
CHUKUA MKOPO WA HARAKA NA UPEWE BONUS YA TSH.10,000/= KWA M-PESA AU TIGOPESA KUPITIA "BRANCH".  Umepata emergency yoyote na unahitaji pesa kwa haraka? Unahitaji mkopo? BRANCH ni Application iliyoanzishwa na Mzungu kutoka Marekani inayotoa mikopo direct kwenye simu yako. Unachohitaji ni kuDownload Application hii na kujaza maswali utakayoulizwa ikiwemo majina yako kamili, namba ya simu, namba ya leseni au kitambulisho cha kazi,taifa, kura, n.k. Mkopo ni instantly unatumiwa kwenye simu yako na wanakupa na repayment period. Application hii inafanya kazi only in Kenya and Tanzania. Trust me these applications dont disappont. Unakuwa na hela sasa hivi. BRANCH inakupa mkopo wa haraka na bonus ya 10,000 baada ya kukopa Namna ya kujiunga : TEMBELEA PLAYSTORE KISHA DOWNLOD "BRANCH" STEP 1 Chagua lugha / Choose Your Language STEP 2 Ukishaifungua app yako ya BRANCH .... Bonyeza NEW ACCOUNT (ACCOUNTMPYA) ipo sehemu ya chini, katika maneno yaliyoandikwa : OR REGEST...

SIMBA WAFUNGWA NA NKANA FC BAO 2-1, ZAMBIA

Image
TIMU ya  Simba imefungwa bao 2-1 dhidi ya Nkana FC kwenye Uwanja wa Nkana, Kitwe, Zambia unaobeba mashabiki 10,000 katika mchezo muhimu wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Mabao ya Nkana FC yamefungwa na Ronald Kampamba dakika ya 27 kipindi cha kwanza na Kelvin Kampamba dakika ya 56 kipindi cha pili. Simba wamepata bao  kupitia kwa John Bocco kwa mkwaju wa penati dakika ya 73 kipindi cha pili baada ya Meddie Kagere kuangushwa kwenye eneo la hatari.

YONDANI: BOBAN KASAINI, WAMEKWISHA

Image
KELVIN Yondani juzi jioni aliwasha WhatsApp yake akaanza kucheka. Washikaji waliokuwa karibu nae wakaanza kujiuliza kulikoni, kwani kuna habari gani? Baadaye akawaambia mwanangu kasaini. Wakawa wanajiuliza mwanae yupi? Akawaonyesha picha ya Haruna Moshi ‘Boban’ akimwaga wino kuichezea Yanga miezi sita. Sasa jana Ijumaa Yondani ambaye ataukosa mchezo wa kesho Jumapili dhidi ya Ruvu Shooting, mwenyewe amezungumza na  Championi Jumamosi  akatamka kwamba katika usajili wa maana ambao Mwinyi Zahera ameufanya msimu huu ni wa Boban. Yondani ambaye ni nahodha wa Yanga aliweka wazi kwamba awali aliusifia usajili wa Mrisho Ngassa baadhi ya watu wakawa wanaguna lakini sasa amewaziba midomo uwanjani. Boban ambaye mpaka sasa amefunga mabao mawili ligi kuu, juzi alisaini mkataba wa miezi sita Yanga kwa dau la Shilingi milioni 25 akitokea African Lyon ambayo hali yao ilivyo tete ni Mungu anajua. Boban aliyewahi kuichezea Simba kwa mafanikio, amesajiliwa na Yanga baad...

WANACHAMA YANGA WAGOMEA UCHAGUZI

Image
MATAWI ya Yanga, Kanda ya Kinondoni wameafikiana kwa pamoja kutoshiriki uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo mwezi ujao, Mwenyekiti wao, Shabani Msonja amethibitisha. “Hatupo tayari kwa uchaguzi ambao TFF watausimamia na kama watatuhitaji sisi Kanda ya Kinondoni, sio peke yetu bali hata kanda nyingine pia hawapo tayari kwa ajili ya uchaguzi,’’alisema mbele ya wanachama wengine kwenye mkutano wao, Magomeni Mwembechai, Jijini Dar es Salaam. “Ndugu zetu Jonas Tiboroha na Mbaraka Igangula wamejitakia matatizo wenyewe maana wanagombea kuiongoza timu kwa mwaka mmoja. We fikiria Yanga na matatizo yetu mwaka mmoja unatosha kufanya maendeleo gani, sasa wajiandae kuja na polisi kila watakapotaka kuingia ndani ya jengo la Yanga,”alisema kiongozi huyo. Msonja ambaye alisema msimamo huo ni wa matawi 45 ya Yanga kwenye Kanda hiyo inayojumuisha na Ubungo.

CHUKUA MKOPO WA HARAKA NA UPEWE BONUS YA TSH.10,000/= KWA M-PESA AU TIGOPESA KUPITIA "BRANCH".

Image
CHUKUA MKOPO WA HARAKA NA UPEWE BONUS YA TSH.10,000/= KWA M-PESA AU TIGOPESA KUPITIA "BRANCH".  Umepata emergency yoyote na unahitaji pesa kwa haraka? Unahitaji mkopo? BRANCH ni Application iliyoanzishwa na Mzungu kutoka Marekani inayotoa mikopo direct kwenye simu yako. Unachohitaji ni kuDownload Application hii na kujaza maswali utakayoulizwa ikiwemo majina yako kamili, namba ya simu, namba ya leseni au kitambulisho cha kazi,taifa, kura, n.k. Mkopo ni instantly unatumiwa kwenye simu yako na wanakupa na repayment period. Application hii inafanya kazi only in Kenya and Tanzania. Trust me these applications dont disappont. Unakuwa na hela sasa hivi. BRANCH inakupa mkopo wa haraka na bonus ya 10,000 baada ya kukopa Namna ya kujiunga : TEMBELEA PLAYSTORE KISHA DOWNLOD "BRANCH" STEP 1 Chagua lugha / Choose Your Language STEP 2 Ukishaifungua app yako ya BRANCH .... Bonyeza NEW ACCOUNT (ACCOUNTMPYA) ipo sehemu ya chini, katika maneno yaliyoandikwa : OR REG...

ZAHERA, MAKAMBO WAKIMBIZA TUZO LIGI KUU

Image
Klabu ya soka ya Yanga kupitia kwa mshambuliaji wake, Heritier Makambo na kocha, Mwinyi Zahera imeibuka kinara kwenye tuzo za mchezaji bora na kocha bora wa mwezi Novemba. Shirikisho la soka nchini (TFF), leo limetangaza mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makambo kuwa mchezaji bora wa mwezi Novemba wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL). Makambo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda nyota wengine Said Dilunga wa Ruvu Shooting na beki Abdallah Shaibu wa Yanga. Aidha kamati ya tuzo hizo pia imemchagua Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera kuwa Kocha Bora wa Novemba akiwashinda Kocha Mkuu wa Coastal Union, Juma Mgunda na Kaimu Kocha Mkuu wa Alliance FC, Gilbert Dadi alioingia nao fainali. Ndani ya mwezi Novemba, Yanga imeshinda mechi 3 dhidi ya Ndanda FC, Mwadui FC na Kagera Sugar huku mchezaji Heritier Makambo akifunga mabao 2 katika mechi hizo.

Munala confirmed at KCB as the bankers sign seven Pipeline players

Image
Coach Kenya Pipeline Women team Japheth Munala (left) and player Agripinah Kundu during National Volleyball playoff tournament at Kasarani stadium on Sunday, Dec 3, 2018. [Jonah Onyango, Standard] After several weeks of speculations, national women’s volleyball team coach Japheth Munala has finally been appointed as KCB head coach. Munala replaces David Muthui, who has been serving on an interim capacity since the sacking of Vernon Khainga a few months ago. This comes barely a week after the experienced coach oversaw Kenya Pipeline relinquish their national title to rivals Prisons Kenya during the Kenya Volleyball League play-offs at the Kasarani Gymnasium. Munala has moved back to the bankers alongside seven key players from his former Embakasi-based side as he begins the club’s rebuilding process ahead of next year’s African Club Championship in Egypt. They are former KVF most valuable player Violet Makuto, Noel Murambi, Jemima Siangu (left attackers), Leonida Kasaya (cent...

Gor Mahia, Sharks head West in next round of matches

Image
Goalkeeper Gor Mahia FC Boniface Oluoch seems to be telling his coaleagues to be on the watchout during KPL Match against AFC at Nyayo National Stadium, Oct 23, 2016. [PHOTO: JONAH ONYANGO/STANDARD] For the first time in many years, two Kenyan clubs have made it to the first round of the Confederation of African Football (CAF) tournament and are lined up for millions after reaching group stages. Gor Mahia needed post-match penalties to edge out Nyasa Big Bullets of Malawi 4-3 in their CAF Champions League preliminary match in Blantyre on Wednesday. The hosts had won the match 1-0 for an aggregate score of 1-1 as Gor Mahia had won the first leg with a similar margin. Kariobangi Sharks edged out Djibouti’s Arta Solar 9-1 on aggregate in the preliminary stage of the Confederations Cup. They had won the first leg 6-1 and followed it up with a 3-0 win in the return match. Kenyan clubs have over the years been struggling to make it past the preliminary stage of the continental foo...

SIMBA YAITUPA NJE MBAMBANE SWALLOWS KWA MABAO 8-1

Image
TIMU ya Simba, leo imeibuka na ushindi  wa bao 4-0 dhidi  ya Mbambane Swallows ya Swaziland katika mchezo wa marudiano wa Mabingwa Afrika . Wafungaji wa Simba katika mechi hiyo ni  Cletus Chama dakika 28 na 33, Emmanuel Okwi  dakika 51 na Meddie Kagere  dakika ya 63. Kwa ushindi huo, Simba wamewatupa nje ya mashindano hayo  Mbambane Swallows kwa jumla ya mabao 8-1. Mechi ya kwanza iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Simba ilishinda mabao 4-1.

BEKI MPYA SIMBA AKABIDHIWA DOZI NENE

Image
BEKI mpya wa Simba, Zana Coulibaly, amefunguka kuwa ameshindwa kusafiri na timu hiyo kwa kuwa hayupo kwenye michuano hiyo, lakini akasema ameachiwa programu maalum ya mazoezi ili kuwa fiti zaidi kabla ya wenzake kurejea. Coulibaly, raia wa Burkina Faso, amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili katika usajili wa dirisha dogo unaotarajiwa kufungwa Desemba 15, mwaka huu lakini hakuweza kusafiri na timu hiyo kwenda nchini Eswatini katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mbabane Swallows kutokana jina lake kutokuwepo kwenye michuano hiyo. Akizungumza na Championi Jumatano, Coulibaly alisema kuwa licha ya kutoshiriki michuano hiyo, ameachiwa programu maalum ya mazoezi anayofanya asubuhi na jioni. “Sijasafiri kwa sababu sichezi mashindano hayo na jina langu bado halijaenda Caf kwa kuwa sikuwepo awali kwenye timu lakini kwa kuwa nimesaini mkataba wa miaka miwili, basi nitacheza huko mbele kwenye hatua nyingine. “Lakini mwalimu ameniachia programu m...

BALLON D’OR: MODRIC AMALIZA UFALME WA MESSI, RONALDO

Image
Mohammed Salah ndiyo mchezaji pekee kutoka Afrika aliyeingia katika 10 bora kwa kushika nafasi ya sita, na ndiyo mchezaji kinara kutoka Ligi ya Premier ya England. Modric alikuwa ni miongoni mwa wachezaji wanane wa Real Madrid kati ya wachezaji 30 waliokuwa wakiwania tuzo hiyo, akiwemo Gareth Bale aliyemaliza katika nafasi ya 17. Mshambuliaji wa Lyon na Norway Ada Hegerberg, 23, ameshinda tuzo ya kwanza ya Ballon d’Or kwa wachezaji wa kike huku Mbappe, 19, akishinda tuzo ya Kopa inayotolewa kwa mchezaji bora chini ya miaka 21 kwa kupigiwa kura na washindi wa zamani wa Ballon d’Or. 10  Bora ya Ballon d’Or 1. Luka Modric (Real Madrid and Croatia) 2. Cristiano Ronaldo (Juventus and Portugal) 3. Antoine Griezmann (Atletico Madrid and France) 4. Kylian Mbappe (Paris St-Germain and France) 5. Lionel Messi (Barcelona and Argentina) 6. Mohamed Salah (Liverpool and Egypt) 7. Raphael Varane (Real Madrid and France) 8. Eden Hazard (Chelsea and Belgium) 9. Kevin de Bruy...

RASMI SONSO AMALIZANA NA YANGA SC

Image
YANGA imelamba dume! Unaweza kusema hivyo baada ya kumalizana na beki wa kati mwenye kiwango cha juu wa Lipuli FC, Ally Mtoni ‘Sonso’, sasa ataungana na kikosi hicho kesho Jumapili. Yanga ilianza mbio za kumuwania mlinzi huyo ambaye alionyesha uwezo mkubwa kwenye mechi ya timu ya taifa, Taifa Stars iliyocheza dhidi ya Lesotho katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Mataifa Afrika. Championi Jumamosi  ambalo lipo mkoani Iringa, lilizungumza na mlinzi huyo ambaye alikuwa na nyota wenzake wa Lipuli kwa mara ya mwisho kabla ya kwenda kuanza maisha mapya pale Yanga jijini Dar. Sonso ambaye ni mrefu na amefuga rasta kichwani mwake, amelihakikishia  Championi Jumamosi  kuwa amemalizana na Yanga na anachosubiri kwa sasa ni viongozi wa Lipuli na Yanga kumalizana kwa ngazi ya uongozi ambao tayari wameanza mazungumzo. “Nimeshamalizana na Yanga, nilikuwa nasubiri viongozi wangu wamalizane na Yanga ili niweze kuondoka. Wameniambia Jumapili ndiyo nitaungana na Yanga...

SIMBA WAWALAZA MBABANE SWALLOWS BAO 4-1

Image
Kikosi cha Simba kimefanikiwa kuanza vizuri leo katika mchezo wa Fainali za Mabingwa ya Afrika uliochezwa Uwanja wa Taifa kwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Mbabane Swallows FC ya Swaziland. Mabao ya Simba yalifungwa na John Bocco dakika ya 7 akimalizia pasi ya Nicolus Gyan kisha akafunga bao la pili dakika ya 32 kwa mkwaju wa penati baada ya Emmanuel Okwi kuchezewa rafu na mlinda mlango wa Mbabane. Mbabane waliweza kutikisa nyavu za Simba dakika ya 24 lililofungwa na Guevane Nzambe na kufanya kipindi cha pili kumalizika kwa bao 2-1. Simba walirejea kwa kasi kipindi cha pili na kufanikiwa kufanya mashambulizi na wakafunga bao la 3 lililofungwa na Meddie Kagere dakika ya 83 baada ya mlinda mlango wa Mbabane kuteleza akiwa na mpira kisha dakika ya 90 Clatous Chama alifunga bao la 4 akimalizia pasi ya Hassan Dilunga. Simba watatakiwa wasiruhusu bao wakienda ugenini ili waweze kusonga mbele katika hatua ya michuano hii kwa kuwa Mbabane sio timu ya kubeza

FEDHA ZA YONDANI ZAZUIA USAJILI YANGA SC

Image
KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ameuambia uongozi wa timu hiyo kuwa hawezi kufanya usajili wa wachezaji wapya kwenye dirisha dogo kwa kuwa wachezaji wake wengi bado wanadai fedha zao za usajili. Zahera mwenye uraia wa DR Congo na Ufaransa ameyasema hayo kufuatia beki wake wa kati, Kelvin Yondani na kipa Beno Kakolanya kugomea kujiunga na timu kufuatia kudai fedha kwenye timu hiyo. Yondani na Kakolanya wamegomea kujiunga na timu wakitokea kwenye kambi ya timu ya taifa, Taifa Stars kuelekea kwenye mechi mbili za Kanda ya Ziwa ambazo zote Yanga ilifanikiwa kushinda. Akizungumza na Championi Jumatano, Zahera alisema kuwa hawezi kufanya usajili wa wachezaji wapya katika usajili wa dirisha dogo iwapo viongozi wa timu hiyo watashindwa kumaliza matatizo ya wachezaji waliopo kwa sasa kwenye kikosi chake. “Kama ukimya basi fahamu kuna tatizo, unajua usajili ni kitu kikubwa, unaweza nyumbani kukawa na matatizo, mtoto wako haendi shule sasa sijui kama unaweza tena kuleta mtoto...

MAKAMBO AMFUNIKA VIBAYA KAGERE

Image
shambuliaji wa Yanga raia wa DR Congo, Heritier Makambo. MAMBO ni moto! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya mshambuliaji wa Yanga raia wa DR Congo, Heritier Makambo kuandika rekodi ya pekee hivi karibuni katika michuano ya Ligi Kuu Bara. Makambo ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kwenye Ligi Kuu Bara kufunga mabao kwenye michezo miwili mfululizo ya mkoani na kuwazidi Emmanuel Okwi pamoja na Mnyarwanda, Meddie Kagere wa Simba. Mnyarwanda, Meddie Kagere wa Simba. Makambo alifunga kwenye mechi dhidi ya Mwadui FC pamoja na Kagera Sugar ambazo zote Yanga walishinda. Ilianza dhidi ya Mwadui FC, Novemba 22, mwaka huu katika Uwanja wa Kambarage Shinyanga na katika mchezo huo Makambo aliifungia timu yake hiyo bao moja kati ya mabao ya mawili iliyoshinda. Baada ya hapo Yanga ilipambana na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba na katika mechi hiyo Makambo alifanikiwa kuifungia timu hiyo kwa mara nyingine bao moja kati ya mabao mawili ambayo iliyapata kwen...

MKUDE, CHAMA WAPEWA KAZI MAALUM KUIUA MBABANE

Image
SIMBA ipo ka­tika maandalizi makali ya mechi yake ya Juma­tano ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mbabane Swal­lows kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, kocha Mbel­giji, Patrick Aussems amewapa kazi maalumu viungo wake wawili,  Jo­nas Mkude na Mzambia, Cletus Chama. Akuzungumza na  Cham­pioni Jumatatu,  Mkude alisema kuwa Aussems amefikia hatua hiyo baada ya kukamilisha uchunguzi wake dhidi ya Mbabane Swallows.Alisema katika uchunguzi huo alibaini kuwa Mbabane wapo vizuri sehemu ya kiungo, ndiyo maana akaamua kuwapatia kazi maalumu. “Kwa sasa tunaendelea kujifua vilivyo ili tuweze kuwa fiti tayari kwa kuifanya kazi hiyo am­bayo kocha ametupatia, ni matumaini yangu kuwa ha­tutamwan­gusha kocha, tutaifan­ya kama anavyotaka. “ Kazi yenyewe hiyo kwa sasa si­wezi kuisema ila kwa yeyote atakayekuja uwanjani siku hiyo ataiona,” alisema Mkude ambaye hucheza nafasi ya kiungo mkabaji akishirikiana vilivyo na Mghana, James Kotei. Kwa upande wake Cha­ma yeye hucheza nafasi ya kiung...

CHIRWA AMKIMBIZA STRAIKA AZAM

Image
U jio wa Obrey Chirwa umesababi­sha Ditram Nchimbi aondolewe katika kikosi cha Azam. Nchimbi alikuwa tegemeo kwenye kikosi cha Njombe Mji iliyoshuka daraja msimu uliiopita wa Ligi Kuu Bara kabla ya kusajiliwa na Azam, lakini ameshindwa kuonyesha kiwango kilichotarajiwa akiwa Azam. Kutua kwa Chirwa kumeongeza idadi ya washambuliaji kufikia sita, wengine wakiwa ni Donald Ngoma, Mbaraka Yusuph, Danny Lyanga, Yahya Zayd na Tafazwa Kutinyu, hiyo ni baa­da ya kuondolewa Nchimbi. Meneja wa timu hiyo, Philipo Alando alisema kuwa wam­emtoa kwa mkopo Nchimbi kwenda ili akapate nafasi ya kucheza WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

KAPOMBE APASULIWA MGUU SAUZ

Image
B EKI wa kulia wa Sim­ba, Shomari Kapombe, amefanyiwa upasuaji wa mguu kufuatia kuu­mia enka kwenye kambi yaT­aifa Stars nchini Afrika Kusini. Beki huyo alikuwa kwenye kambi ya timu hiyo iliyokuwa ina­jiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu Afcon dhidi ya Lesotho katika mchezo uliopigwa nchini Lesotho, wikiendi iliopita. Beki huyo ambaye alilazimika kubakia nchini humo kwa ajili ya kupatiwa matibabu, juzi alifanyi­wa upasuaji wa mguu wake katika hospitali moja kubwa kwenye Jiji la Pretoria, Afrika Kusini. Akizungumza na  Championi Jumatatu,  mwenyekiti wa timu hiyo, Swedy Mkwabi alisema up­asuaji huo utamlazimu Kapombe kukaa nje ya uwanja kwa wiki sita. “Kesho Jumatatu (leo) atak­wenda tena hospitali kuonana na daktari wake ili kuangalia maen­deleo baada ya upasuaji kwa sababu atakuwa nje kwa muda wa wiki sita isipokuwa atarejea nchini wakati wowote kulingana na dak­tari wake atakavyokuwa ameon­gea naye,” alisema Mkwabi. WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

MBELGIJI SIMBA: NIMEPEWA JINA LA ULIMWENGU

Image
KOCHA  wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems ameweka wazi kuwa amekabidhiwa jina la mshambuliaji Thomas Ulimwengu. Ulimwengu ambaye amevunja mkataba wake na Al Hilal ya Sudan anatajwa kutakiwa na Simba kwa ajili ya kumtumia kwenye michuano ya kimataifa. Mshambuliaji huyo alikuwa na Taifa Stars nchini Lesotho katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa Afrika lakini hakuweza kucheza kutokana na kocha mkuu wa timu hiyo, Mnigeria, Emmanuel Amunike kumuweka benchi. Ulimwengu amecheza mechi mbili tu chini ya Amunike ambazo zilikuwa ni dhidi ya Uganda na ile mechi ya kwanza ya Cape Verde, hivyo Mbelgiji alitegemea amuone akicheza na Lesotho lakini haikuwa hivyo. Awali chanzo makini kutoka ndani ya Simba, kililiambia  Championi Jumamosi  kuwa, klabu hiyo ilikuwa kwenye mchakato wa kutaka kumsaini lakini kwa sasa inaonekana kama unaelekea kukwama kutokana na kocha kutomuona Ulimwengu akicheza licha ya kuambiwa ni mchezaji mzuri. “Usajili wa Ulimwengu bado ...