BALLON D’OR: MODRIC AMALIZA UFALME WA MESSI, RONALDO


Mohammed Salah ndiyo mchezaji pekee kutoka Afrika aliyeingia katika 10 bora kwa kushika nafasi ya sita, na ndiyo mchezaji kinara kutoka Ligi ya Premier ya England.
Modric alikuwa ni miongoni mwa wachezaji wanane wa Real Madrid kati ya wachezaji 30 waliokuwa wakiwania tuzo hiyo, akiwemo Gareth Bale aliyemaliza katika nafasi ya 17. Mshambuliaji wa Lyon na Norway Ada Hegerberg, 23, ameshinda tuzo ya kwanza ya Ballon d’Or kwa wachezaji wa kike huku Mbappe, 19, akishinda tuzo ya Kopa inayotolewa kwa mchezaji bora chini ya miaka 21 kwa kupigiwa kura na washindi wa zamani wa Ballon d’Or.
10 Bora ya Ballon d’Or
1. Luka Modric (Real Madrid and Croatia)
2. Cristiano Ronaldo (Juventus and Portugal)
3. Antoine Griezmann (Atletico Madrid and France)
4. Kylian Mbappe (Paris St-Germain and France)
5. Lionel Messi (Barcelona and Argentina)
6. Mohamed Salah (Liverpool and Egypt)
7. Raphael Varane (Real Madrid and France)
8. Eden Hazard (Chelsea and Belgium)
9. Kevin de Bruyne (Manchester City and Belgium)
10. Harry Kane (Tottenham and England)
Ballon d’Or ni nini?
Tuzo ya Ballon d’Or imekuwa ikitolewa nchini Ufaransa kila mwaka toka 1956, na msindi wake wa kwanza alikuwa mchezaji kutoka Uingereza Stanley Matthews. Tuzo hiyo awali ilikuwa ni kwa wachezaji wa Ulaya tu kabla ya kufanyika mabadiliko mwaka 1995 na kujumuisha wachezaji wa mataifa yote duniani, mradi wanasakata kandanda katika vilabu vya Ulaya.
Orodha ya majina ya wachezaji 30 bora huandaliwa na baadaye kupigiwa kura na wanahabari wa michezo kutoka sehemu tofauti duniani, ambapo kila nchi hupiga kura moja. Kutoka mwaka 2010 mpaka 2015 tuzo hiyo iliunganishwa na ile ya Fifa lakini zilitengana mwaka 2016 ambapo Fifa ilianza kuandaa tuzo zake.
Washindi wa Ballon d’Or : Ronaldo & Messi walitawala kuanzia 2008
2007KakaCristiano RonaldoLionel Messi
2008Cristiano RonaldoLionel MessiFernando Torres
2009Lionel MessiCristiano RonaldoXavi
2010Lionel MessiAndres IniestaXavi
2011Lionel MessiCristiano RonaldoXavi
2012Lionel MessiCristiano RonaldoAndres Iniesta
2013Cristiano RonaldoLionel MessiFranck Ribery
2014Cristiano RonaldoLionel MessiManuel Neuer
2015Lionel MessiCristiano RonaldoNeymar
2016Cristiano RonaldoLionel MessiAntoine Griezmann
2017Cristiano RonaldoLionel MessiNeymar
2018Luka ModricCristiano RonaldoAntoine Griezmann

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!