BEKI MPYA SIMBA AKABIDHIWA DOZI NENE



BEKI mpya wa Simba, Zana Coulibaly, amefunguka kuwa ameshindwa kusafiri na timu hiyo kwa kuwa hayupo kwenye michuano hiyo, lakini akasema ameachiwa programu maalum ya mazoezi ili kuwa fiti zaidi kabla ya wenzake kurejea.
Coulibaly, raia wa Burkina Faso, amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili katika usajili wa dirisha dogo unaotarajiwa kufungwa Desemba 15, mwaka huu lakini hakuweza kusafiri na timu hiyo kwenda nchini Eswatini katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mbabane Swallows kutokana jina lake kutokuwepo kwenye michuano hiyo.
Akizungumza na Championi Jumatano, Coulibaly alisema kuwa licha ya kutoshiriki michuano hiyo, ameachiwa programu maalum ya mazoezi anayofanya asubuhi na jioni.

“Sijasafiri kwa sababu sichezi mashindano hayo na jina langu bado halijaenda Caf kwa kuwa sikuwepo awali kwenye timu lakini kwa kuwa nimesaini mkataba wa miaka miwili, basi nitacheza huko mbele kwenye hatua nyingine.

“Lakini mwalimu ameniachia programu maalum kwa ajili ya kufanya mazoezi ambayo naifanyia ufukweni asubuhi na jioni ili kuniweka fiti na hata watakaporejea basi niweze kwenda sawa na mazoezi mengine,” alisema Coulibaly

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!