SIMBA WAFUNGWA NA NKANA FC BAO 2-1, ZAMBIA
TIMU ya Simba imefungwa bao 2-1 dhidi ya Nkana FC kwenye Uwanja wa Nkana, Kitwe, Zambia unaobeba mashabiki 10,000 katika mchezo muhimu wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mabao ya Nkana FC yamefungwa na Ronald Kampamba dakika ya 27 kipindi cha kwanza na Kelvin Kampamba dakika ya 56 kipindi cha pili.
Simba wamepata bao kupitia kwa John Bocco kwa mkwaju wa penati dakika ya 73 kipindi cha pili baada ya Meddie Kagere kuangushwa kwenye eneo la hatari.
Comments
Post a Comment