SIMBA YAITUPA NJE MBAMBANE SWALLOWS KWA MABAO 8-1
TIMU ya Simba, leo imeibuka na ushindi wa bao 4-0 dhidi ya Mbambane Swallows ya Swaziland katika mchezo wa marudiano wa Mabingwa Afrika . Wafungaji wa Simba katika mechi hiyo ni Cletus Chama dakika 28 na 33, Emmanuel Okwi dakika 51 na Meddie Kagere dakika ya 63.
Kwa ushindi huo, Simba wamewatupa nje ya mashindano hayo Mbambane Swallows kwa jumla ya mabao 8-1. Mechi ya kwanza iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Simba ilishinda mabao 4-1.
Comments
Post a Comment