WANACHAMA YANGA WAGOMEA UCHAGUZI



MATAWI ya Yanga, Kanda ya Kinondoni wameafikiana kwa pamoja kutoshiriki uchaguzi Mkuu wa
klabu hiyo mwezi ujao, Mwenyekiti wao, Shabani Msonja amethibitisha.

“Hatupo tayari kwa uchaguzi ambao TFF watausimamia na kama watatuhitaji sisi Kanda ya Kinondoni, sio peke yetu bali hata kanda nyingine pia hawapo tayari kwa ajili ya uchaguzi,’’alisema mbele ya wanachama wengine kwenye mkutano wao, Magomeni Mwembechai, Jijini Dar es Salaam.

“Ndugu zetu Jonas Tiboroha na Mbaraka Igangula wamejitakia matatizo wenyewe maana wanagombea kuiongoza timu kwa mwaka mmoja. We fikiria Yanga na matatizo yetu mwaka mmoja unatosha kufanya maendeleo gani, sasa wajiandae kuja na polisi kila watakapotaka kuingia ndani ya jengo la Yanga,”alisema kiongozi huyo. Msonja ambaye alisema msimamo huo ni wa matawi 45 ya Yanga kwenye Kanda hiyo inayojumuisha na Ubungo.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!