ZAHERA, MAKAMBO WAKIMBIZA TUZO LIGI KUU
Klabu ya soka ya Yanga kupitia kwa mshambuliaji wake, Heritier Makambo na kocha, Mwinyi Zahera imeibuka kinara kwenye tuzo za mchezaji bora na kocha bora wa mwezi Novemba.
Shirikisho la soka nchini (TFF), leo limetangaza mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makambo kuwa mchezaji bora wa mwezi Novemba wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL).
Makambo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda nyota wengine Said Dilunga wa Ruvu Shooting na beki Abdallah Shaibu wa Yanga.
Aidha kamati ya tuzo hizo pia imemchagua Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera kuwa Kocha Bora wa Novemba akiwashinda Kocha Mkuu wa Coastal Union, Juma Mgunda na Kaimu Kocha Mkuu wa Alliance FC, Gilbert Dadi alioingia nao fainali.
Ndani ya mwezi Novemba, Yanga imeshinda mechi 3 dhidi ya Ndanda FC, Mwadui FC na Kagera Sugar huku mchezaji Heritier Makambo akifunga mabao 2 katika mechi hizo.
Comments
Post a Comment