YONDANI: BOBAN KASAINI, WAMEKWISHA



KELVIN Yondani juzi jioni aliwasha WhatsApp yake akaanza kucheka. Washikaji waliokuwa karibu nae wakaanza kujiuliza kulikoni, kwani kuna habari gani?

Baadaye akawaambia mwanangu kasaini. Wakawa wanajiuliza mwanae yupi? Akawaonyesha picha ya Haruna Moshi ‘Boban’ akimwaga wino kuichezea Yanga miezi sita.

Sasa jana Ijumaa Yondani ambaye ataukosa mchezo wa kesho Jumapili dhidi ya
Ruvu Shooting, mwenyewe amezungumza na Championi Jumamosi akatamka kwamba katika usajili wa maana ambao Mwinyi Zahera ameufanya msimu huu ni wa Boban.
Yondani ambaye ni nahodha wa Yanga aliweka wazi kwamba awali aliusifia usajili wa Mrisho Ngassa baadhi ya watu wakawa wanaguna lakini sasa amewaziba midomo uwanjani.

Boban ambaye mpaka sasa amefunga mabao mawili ligi kuu, juzi alisaini mkataba wa miezi sita Yanga kwa dau la Shilingi milioni 25 akitokea African Lyon ambayo hali yao ilivyo tete ni Mungu anajua.

Boban aliyewahi kuichezea Simba kwa mafanikio, amesajiliwa na Yanga baada ya kocha wake Mkongo, Mwinyi Zahera kutoa mapendekezo ya usajili wake kwa uongozi ili asajiliwe.

Yondani alisema, katika timu lazima wawepo wakongwe watakaofanikisha ubingwa wa ligi kutokana na uzoefu waliokuwa nao pale timu inapotafuta pointi tatu hii ni sawa na kusema wapizani wamekwisha.

“Kama unakumbuka msimu uliopita timu yetu ilikuwa ina watoto wengi hali iliyosababisha tuukose ubingwa kutokana na kukosa uzoefu wakati timu ikipambana kupata matokeo mazuri.

“Niliwahi kuwashauri viongozi tusajili wachezaji wakongwe kama akina Boban wenye uzoefu na watakaobadilisha matokeo ndani ya uwanja, hivyo nashukuru wamelifanyia kazi hilo katika usajili wa msimu huu.

“Utaona walianza kumsajili Ngassa leo hii utaona mchango mkubwa anautoa katika timu kuzidi hao vijana aliowakuta katika timu, hivyo inahitaji pongezi katika hilo,” alisema Yondani ambaye aliwahi kucheza na Boban ndani ya Simba, Taifa Stars na Kilimanjaro Stars.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!