YANGA 4-0 NJOMBE MJI UWANJA WA UHURU



FULL TIME
Mwamuzi anamaliza mchezo, Yanga inapata ushindi wa mabao 4-0.
Dakika ya 93: Mchezo unaweza kumalizika muda wowote kuanzia sasa.
Dakika ya 90: Zinaonyeshwa dakika 3 za nyongeza.
Dakika ya 88: Chirwa anatoka nje, anaingia chipukizi Said.
Dakika ya 88: Mashabiki wa Yanga wanaongeza nguvu ya kushangilia.
Chirwa anaipatia Yanga bao la nne, anamalizia pasi nzuri ya Akilimali.
Dakika ya 87: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dakika ya 83: Akilimali wa Yanga anaingia, anatoka Emmanuel Martine.
Dakika ya 82: Njombe wamepunguza kasi.
Dakika ya 80: Yanga wanapata kona. Mahadhi anapiga inaokolewa.
Dakika ya 75: Yanga wanapata kona, inapigwa inaokolewa.
Dakika ya 73: Njombe wanajaribu kupambana kupata nafasi ya kusawazisha.
Yanga wanapata bao la tatu, mfungaji ni Emmanuel Martine
Dakika ya 68: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dakika ya 67: Yanga wanaongeza kasi ya kushambulia.
Dakika ya 64: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Yanga wanapata penati baada ya beki wa Njombe Mji kuunawa mpira, Anaenda kupiga Chirwa.
Dakika dakika ya 60: Mabadiliko kwa Njombe Mji, Wingenge anatoka, anaingia Kisu,
Dakika ya 57: Juma Mahadhi wa Yanga anaingia, anatoka Raphael Daudi.
Dakika ya 55: Yanga wanajiandaa kupiga faulo.
Dakika ya 54: Kipa wa Njombe Mji, Mbululo anapewa kadi nyekundu baada ya kuudaka mpira nje ya eneo la 18 baada ya kurudishiwa mpira kwa kichwa na mwenzake.
Dakika ya 53: Yanga wanajipanga, wanapata faulo, anapiga Yondani.
Dakika ya 52: Yanga wanafika langoni lakini inakuwa offside.
Chirwa anaipatia Yanga bao la kwanza.
Dakika ya 46: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Yanga wameanza wakionekana kuwa na uimara zaidi ya ilivyokuwa mwanzo
Kipindi cha pili kimjeanza.
MAPUMZIKO
Mwamuzi anakamilisha kipindi cha kwanza.
Inaongezwa dakika moja ya ziada.
Dakika ya 45: Yanga bado wanapata upinzani mkali kutoka kwa Njombe.
Dakika ya 43: Yanga wanapata kona lakini haizai matunda.
Dakika ya 40: Njombe wanatulia na kushambulia.
Dakika ya 39: Kuna mchezaji wa Njombe yuko chini, ameumia, inakuwa faulo.
Dakika ya 17: Gadiel Michael anapiga krosi nzuri hakuna mchezaji wa Yanga wa kuimalizia.
Dakika ya 34: Yanga wanapata kona, anapia Mwashiuya inaokolewa.
Dakika ya 31: Kipa wa Yanga, Kabwili nafanya kazi nzuri ya kuokoa nafasi hatari, inakuwa kona.
Dakika ya 30: Yanga wanafanya shambulizi lakini inaokolewa.
Dakika ya 27: Kiungo wa Yanga, Tshishimbi anapambana katikati.
Dakika ya 25: Yanga wanafanya shambulizi kali, linbapigwa shuti kali linamzidi kipa lakini walinzi wanauwahi mpira.
Dakika ya 24: Kambole wa Njombe anatifuana na Kessy wa Yanga.
Dakika ya 21: Mchezo unaendelea kwa timu ozte kupeana zamu kumiliki mchezo.
Dakika ya 17: Yanga wanaongeza nguvu ya kushambulia.
Dakika ya 15: Yanga wanafanya shambulizi lakini kioa wa Njombe anachezewa faulo.
Dakika ya 9: Njombe wanapiga pasi nyingi katikati ya uwanja.
Dakika ya 5: Njombe Mji wanajipanga taratibu.
Dakika ya 1: Yanga wameanza kwa kasi.
Mchezo umeanza. 
Huu ni mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, unachezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaa, Yanga ni mwenyeji wa Njombe Mji.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!