KAMA KAWA HAJI MANARA HAWEZI KUWAACHA YANGA HIVIHIVI
Simba na Yanga zipo nje ya mipaka ya Tanzania kwa ajili ya michezo yao ya kimataifa iliyopo chini ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), lakini huku nyuma hawajaondoka hivihivi.
Kama kawaida yake Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ametumia ukurasa wake wa Instagram kuwafanyia utani wapinzani wao wa jadi, Yanga kutokana na kuondoka nchini wakiwa wamevaa kaptura huku mmoja wa wachezaji wa Yanga akionekana ameshusha kaptura yake kwa chini kwa staili maarufu ya ‘kata K’.
Manara aliweka picha ambayo inawaonyesha wachezaji wa Yanga wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kisha akaandika ujumbe huu:
“Tofauti ya jumlisha na Msalaba...Tofauti ya Tende na Mende, malizia na tofauti ya Jua na Mvua......kupanga ni kuchagua......”
Baada ya hapo akaandika: “Loooh hizi kata K zingine bana! Boxer nje nje...ila ndiyo ukimataifa huo au siyo! Swap uone tofauti yao na yetu...au sisi tunapendelewa hivi vifaa?🤔🙇”
Aidha, Manara aliamua kuweka picha nyingine kadhaa zikiwaonyesha wachezaji wa Simba wakati wanaondoka kwenye uwanja huo wa ndege pamoja na zile za Yanga ambapo wote waliondoka siku moja ya Jumapili katika katika muda tofauti.
Simba wao wapo Djibouti kucheza dhidi ya Gendarmerie Nationale katika Kombe la Shirikisho, wakati Yanga wapo Shelisheli kukipiga dhidi ya St Louis kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Comments
Post a Comment