MFARANSA WA SIMBA AZUNGUMZIA POINTI 7..................
Kocha Mkuu wa Simba, Pierre Lechantre amesema utofauti wa pointi tano dhidi ya Azam FC na saba dhidi ya Yanga hautakiwiki kuchukuliwa kama sehemu ya timu yake kujihakikishia ubingwa badala yake kuna kazi kubwa inakuja mbele yao.
Simba inaongoza katika Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2017/18 ikiwa na pointi 35 ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 30 kisha Yanga ikiwa na pointi 28.
Lechantre amesema ushindani anaouona kwenye ligi ya Tanzania ni mgumu na amewataka wachezaji wake kuhakikisha kila mmoja anatekeleza majukumu yake ili kutimiza lengo lao la ubingwa.
"Kuwa pointi saba mbele ya wapinzani wetu haijalishi sana kama ndiyo tumemaliza kazi, kwa aina ya ushindani ambao nimeuona, naamini kila mmoja anahitaji kujituma na na kutimiza majukumu yake," alisema Lechantre ambaye ni raia wa Ufaransa.
Comments
Post a Comment