SIKIA HABARI YA OKWI?


Image result for okwi simba sc
Baada ya kuendelea kuwasha moto kwenye Ligi Kuu ya Vodacom, mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi, ameelezea juu ya mipango yake katika ngazi ya kimataifa akiwa na kikosi chake hicho cha Simba.
Okwi ambaye ni raia wa Uganda ameeleza kuwa anajipanga kuhamishia mabao yake katika michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Ifahamike kuwa hadi sasa Okwi ameshafunga mabao 12 katika ligi kuu ya msimu huu na kuchangia Simba kuwa kileleni kwa muda mrefu.
 Akizungumza wakati wa mazoezi ya Simba yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar, Okwi alisema anaamini akifunga mabao mengi timu yake itakuwa na nafasi nzuri ya kufanya vizuri na kuiwezesha kusonga mbele.
Okwi amesisitiza kuwa michuano ya kimataifa ni muhimu na mchezo wao dhidi ya wapinzani wao kutoka nchini Djibouti  utakuwa mwanzo wa wao kufanya vizuri ngazi ya kimataifa.
Katika orodha ya wafungaji wa ligi kuu, Okwi anaongoza akiwa na mabao 12 akifuatiwa na Obrey Chirwa wa Yanga ambaye yupo sawa na John Bocco wa Simba, Habib Haji wa Mbao FC na Mohamed Rashid ambao wote wana mabao saba kila mmoja.
Simba itashiriki michuano hiyo ya kimataifa ambapo watacheza dhidi ya Gendarmerie Tnale ya Djibouti katikia hatua ya awali, mchezo wa kwanza ukitawajiwa kuchezwa katikati ya mwezi huu wa pili.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!