MZEE MWINYI ATENGUA KAULI YA TANZANIA NI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU


Baada ya kupita miaka mingi, hatimaye, rais mstaafu wa awamu ya pili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ali Hassan Mwinyi ametengua kauli yake juu ya soka la Tanzania.
Mzee Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika (Caf), kati ya Simba dhidi ya Gendarmerie ulioshuhudiwa Simba ikipata ushindi wa mabao 4-0.
Mzee Mwinyi alivutiwa na soka la Simba lililoonyeshwa kwenye mchezo huo na baada ya mechi alifuta kauli yake aliyoitoa miaka 30 iliyopita aliposema “Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu” .
Akizungumza baada ya mchezo huo wa jana uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Mzee Mwinyi alisema: 
“Nimeshuhudia mchezo mzuri na sasa nafuta lile neno kwamba Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu kila anaetaka kujifunza kunyoa atunyoe sisi, sasa nyie ndio vinyozi.”

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!