MANENO YA KOCHA WA SINGIDA UNITED


Licha ya kufanikiwa kuiwezesha timu yake kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho, bado Kocha Mkuu wa
Singida United, Hans van Der Pluijm amewatolea ‘povu’ Green Warriors.
Kocha huyo ambaye ni raia wa Uholanzi amesema kuwa Green ambao ndiyo waliocheza nao katika mchezo huo wa Hatua ya 32 Bora, walitumia mbinu ya kujilinda na kucheza rafu nyingi kwa wachezaji wake kiasi kilichochangia wasiweze kupata ushindi walipocheza nao.
Singida United walicheza dhidi ya Green Warriors kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar ambapo Singida walishinda kwa penati 4-3 baada ya matokeo ya sare katika dakika 90 za kawaida.
Kocha huyo wa zamani wa Yanga amelalamika kuwa Green hawakucheza soka la kuelewa, huku akidai kuwa walikuwa wakitumia nguvu kubwa na zikachangia kupoteza burdani ya mchezo huo.
Amesema anashukuru kuona timu yake imepata ushindi katika mchezo huo lakini kinacho muuma ni mbinu za wapinzani wao hao ambao waliwatoa Simba katika hatua ya nyuma kwenye michuano hiyo kwa njia ya penati, mchezo ambao ulifanyika kwenye uwanja huohuo wa Chamazi.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!