WACHEZAJI WA GHANA WAWEKA REKODI MECHI YA SIMBA DHIDI YA AZAM FC
Mchezo wa Simba dhidi ya Azam FC uliopigwa jana kwenye Uwanja wa Taifa bado ni gumzo.
Mtanange huo wa Ligi Kuu ya Vodacom ulimalizika kwa Simba kupata ushindi wa bao 1-0 mfungaji akiwa ni Emmanuel Okwi.
Pamoja na ushindi huo, kulikuwa na gumzo lingine la wachezaji raia wa Ghana kutawal katika wachezaji walioingia uwanjani.
Jumla ya wachezaji nane raia wa Ghana walicheza mchezo huo, idadi kubwa ya wachezaji wa kigeni kucheza kwa pamoja katika mchezo mmoja.
James Kotei na Asante Kwasi walianza katika kikosi cha kwanza cha Simba huku Razak Abarola, Daniel Amoa, Yakubu Mohamed na Enock Atta-Agyei walikuwa kwenye timu iliyoanza kwa upande wa Azam.
Baadaye Azam FC walifanya mabadiliko kwa kumuingiza Bernard Arthur (raia wa Ghana) kuchukua nafasi ya Yahya Zayd na Simba walimtoa Okwi nafasi yake ikachukuliwa na Nicholas Gyan (raia wa Ghana) ambao walikamilisha idadi ya waghana nane kucheza mechi hiyo.
Kwa sheria na kanuni za soka, zinaruhusu timu kucheza mechi ikiwa na wachezaji wasiopungua saba (idadi ya chini kabisa) lakini pia wasizidi 11 (idadi ya juu zaidi), kwa maana hiyo raia hao wa Ghana wangeunda kikosi chao cha wachezaji nane.
Comments
Post a Comment