BOCCO NDIYE MSHAMBULIAJI BORA TANZANIA
Simba imeendea kuwa na mwendelezo mzuri katika msimu huu wa 2017/18, ambapo inaongoza Ligi Kuu ya Vodacom na imeanza kwa kishindo katika Kombe la Shirikisho Afrika, lakini nyuma ya pazia kuna wachezaji ambao wamekuwa wakionyesha uwezo wa juu.
Kuna wachezaji kadhaa wa timu hiyo ambao wameonyesha ni msaada wa Simba kwa safari hii, baadhi yao ni Emmanuel Okwi na Asante Kwasi, lakini kuna mtu anaitwa John Bocco huyu amekuwa akiwakosha mashabiki wengi wa Msimbazi kwa kasi yake ya kutupia.
Mchambuzi wa masuala ya soka nchini Tanzania, Edo Kumwembe amemzungumzia mshambuliaji huyo wa Simba, John Bocco kwa kusema kuwa ndiye mshambuliaji bora kuliko wote kwa sasa nchini Tanzania kwa wazawa.
Edo amesema hayo alipokuwa akichambua michezo leo asubuhi katika kituo cha Radio cha EFM ambapo alisema Bocco anastahili sifa hizo kwa kile ambacho amekuwa akikionyesha.
“Ukiondoa kina Mbwana Samatta na Simon Msuva ambao wapo nje ya Tanzania, kwa sasa Bocco ndiye mchezaji bora kwa washambuliaji wa Tanzania wazawa, amefanya mambo mengi mazuri na bado hajafikia kile kiwango ambacho alikuwa akikionyesha alipokuwa Azam FC.
“Bocco anafunga na anawapagawisha mashabiki wa Simba lakini kama akifikia ule ubora aliokuwa akiuonyesha alipokuwa Azam naamini mashabiki wa Simba watapagawa zaidi,” alisema Edo Kumwembe.
Comments
Post a Comment