AFYA YA EMMANUEL OKWI KABLA YA MCHEZO WA AZAM FC HAYA HAPA…
Siku moja kabla ya kuivaa Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, kuna taarifa
nzuri kwa mashabiki wa Klabu ya Simba.
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha timu yake ambacho kitacheza mchezo wa kesho Jumatano dhidi ya Azam FC baada ya kuwa na hofu kuwa atakosekana.
Okwi alishindwa kuendelea na mchezo wa timu yake dhidi ya Ruvu Shootingi katika kipindi cha kwanza baada ya kuumizwa shingoni na Mau Bofu wa Ruvu.
Daktari wa Simba, Yassin Gembe amesema kuwa mchezjai wakeyuko fiti na hakupata majeraha makubwa, hivyo yupo kambini pamoja na wenzake kwa ajili ya mchezo huo.
Comments
Post a Comment