Posts

Showing posts from 2019

Lwandamina Amvulia Kofia Yondani

Image
Kelvin Yondani BEKI kisiki wa Yanga, Kelvin Yondani, anaonekana kuwa tishio mbele ya kikosi cha Zesco United baada ya kocha mkuu wa kikosi hicho, Mzambia, George Lwandamina, kuweka wazi kuwa, beki huyo ni miongoni mwa mabeki bora ambao amewahi kuwafundisha. Kauli ya Lwandamina imekuja zikiwa zimebaki siku chache kabla ya Yanga haijavaana na Zesco United katika mchezo wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Yanga na Zesco United zitaumana Septemba 14, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa raundi ya kwanza wa michuano hiyo, kabla ya kurudiana Septemba 27, mwaka huu nchini Zambia. Akizungumza na Championi Jumatano, Lwandamina ambaye aliwahi kuinoa Yanga kabla ya kuondoka wakati msimu wa 2017/18 ukielekea ukingoni, alisema, anamkubali beki huyo kuwa ni miongoni mwa walinzi bora ambao amewahi kuwafundisha. “Niliwahi kuwa Kocha wa Yanga, kwa hiyo Kelvin Yondani namfahamu vizuri kuwa ni beki mzuri, hilo halina ubishi, ni moja ya bek...

Zahera afumua kikosi chote Yanga

Image
Kikosi cha yanga kilichofungwa na Polisi Tanzania KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera ameamua kufumua kikosi chote huku akisisitiza kwamba hafanyi mambo kufurahisha mashabiki. Zahera amekwenda mbali na kusisitiza kwamba hata katika mechi ya kirafiki leo Jumapili dhidi ya AFC Leopards hakuna hata mchezaji mmoja aliyecheza Moshi dhidi ya Polisi Tanzania atakayeanza. Katika mechi dhidi ya Polisi juzi Ijumaa Yanga ilifungwa mabao 2-0 huku ikianzisha sura nyingi mpya. Zahera amekwenda mbali zaidi kwa kusema kwamba hata kwenye mechi ya marudiano dhidi ya Township Rollers hakuna mchezaji yoyote aliyecheza dhidi ya Polisi ataanza. Kikosi cha kwanza kilichoanza dhidi ya Polisi kilikuwa na Ramadhani Kabwili,Mustafa Seleman,Gustava Saimon,Ally Ally,Kelvin Yondani,Abdulaziz Makame,Maybin Kalengo,Feisal Salum,David Molinga na Deus Kaseke. Kocha huyo anayezungumzia Kiswahili cha lafudhi ya Kicongo amesisitiza kwamba anakifanyia mabadiliko makubwa kikosi hicho ili kupata ubora ana...

La Galaxy Wampa Ninja Namba 51

Image
 BEKI wa zamani wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ juzi Ijumaa alitambulishwa rasmi katika mtandao wa klabu ya La Galaxy II kama mchezaji wa timu hiyo huku akiwa amepewa jezi namba 51. Ninja amejiunga na timu kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea katika timu ya MFK Vyskov ya Jamhuri ya Czech baada ya kumaliza mkataba wake wa miwili na Yanga akiwa ametokea Taifa Jang’ombe ya Zanzibar. Ninja alitambulishwa katika mtandao rasmi wa timu hiyo ambao unahusika kutoa taarifa za timu hiyo anayocheza mshambuliaji wa zamani wa Barcelona na Manchester United, Zlatan Ibrahimović. Akizungumza na mtandao huo, meneja mkuu wa timu hiyo, Dennis te Kloese alisema kuwa wamesaini beki huyo kutoka Tanzania kwa mkataba wa mkopo wa muda mrefu akitokea katika klabu ya MFK Vyskov huku akiwa tayari ameshapa kibali chake cha uhamisho wa kimataifa ITC na kibali cha kufanyia kazi nchini maarufu kama P1 Visa. “Tumemsajili Abdalla (Ninja) katika orodha ya wachezaji wetu kwa ajili msimu ujao...

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

Image
 NAHODHA wa timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’, Mbwana Samatta amefunga mabao matatu (hat-trick), katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza nchini Ubelgiji dhidi ya Waasland-Beveren. Samatta aliiongoza klabu ya KRC Genk kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 katika mchezo huo uliochezwa juzi, kwenye Uwanja wa Freethielstadion, mjini Beveren. Mshambuliaji huyo alifunga mabao hayo, dakika za 53, 66 na 86, huku bao jingine likifungwa na Joseph Paintsil dakika ya 21. Samatta anakuwa mshambuliaji wa tatu kufikisha mabao manne, baada ya kucheza michezo minne ya ligi hiyo msimu huu, wengine ni Dieumerci Mbokani wa Royal Antwerp na David Okereke wa Club Brugge. Huo ni mwanzo mzuri kwa Samatta ambaye msimu uliopita aliimaliza nafasi ya pili kwenye chati ya wafungaji bora wa ligi hiyo , akiwa na mabao 23, mabao mawili nyuma ya Hamdi Harbaoui wa Zulte Waregem aliyechukua kiatu cha ufungaji bora. Samatta sasa amefikisha mabao 66, katika mechi ya 160 za mashindano yote, t...

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!

Image
 ACHANA na mechi ya Man city na Spurs, ngoma leo saa 1 usiku iko kwenye Uwanja wa Taifa kwa Simba na azam. Kwa lugha rahisi ni kwamba wenye mpira wao Tanzania wanafungua msimu mpya kwa burudani ya Ngao ya Jamii. Kuanzia nje mpaka ndani ya Uwanja hizi ndizo klabu zenye bajeti kubwa zaidi na leo zinakutana Taifa kuonyeshana ubabe na kufungua njia mpya. Ni mechi ngumu na itakayokuwa na utamu wa aina yake. Ni lazima mtu akae, hakuna cha sare wala suluhu. Mtaalam Razack Abalora atasimama kwenye lango la Azam huku pembeni katika ulinzi wakisimama Nicholas Wadada na Bruce Kangwa. Pale kati atakuwepo Daniel Amoah na Oscar Masai. Kati yupo Yakub Mohammed, Abdallah Masoud, Salmin Hoza, Salum Aboubakary ‘Sure Boy’ na Idd Seleman. Huyu ni wakuitwa Nado. Pale mbele anamalizia Obrey Chirwa mwenyewe. Simba sasa. Aishi Manula hayuko fiti. Beno Kakolanya ataanza chini ya ulinzi wa Shomari Kapombe,Hussein Mohammed ‘Tshabalala’, Pascal Wawa na Tairone Dos Santos. Kuna mtu ...

Passport Yamuondoa Balama

Image
 IDARA ya Uhamiaji Tanzania imemzuia kiungo mshambuliaji mpya wa Yanga, Mapinduzi Balama kujiunga na kambi ya kujiandaa na mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Yanga imeingia kambini Jumanne ya wiki hii huko Chuo cha Mwika Wildlife kilichopo Moshi, Kilimanjaro ambako inajiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Township Rollers ya Botswana. Timu hizo zinatarajiwa kucheza mchezo huo wa marudiano Agosti 24, mwaka huko Botswana baada ya awali kutoka sare ya kufungana bao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar. Mratibu wa timu hiyo, Hafidh Saleh amesema kuwa, kiungo huyo aliachwa Dar kwa ajili kukamilisha kibali cha kusafiria kinachosimamiwa na Idara ya Uhamiaji. “Balama yupo njiani, hapa ninavyozungumza na wewe, tulishindwa kuja naye ili akamilishe hati yake ya kusafiria. “Ilikuwa lazima tumuache Dar ili ajiunge na wenzake baada ya kocha kuutaka uongozi ukamilishe haraka hati yake ya kusafiria tayari kwa safari ya Botswana. “Hivyo, Balama yup...

Rage: Kwa Deo Kanda, Kahata Simba SC Imelamba Dume

Image
 ISMAIL Aden Rage ambaye ni mwenyekiti wa zamani wa Simba, ameweka wazi kuwa timu hiyo imelamba dume kwa kuwasajili mshambuliaji Deo Kanda na kiungo Francis Kahata. Deo Kanda amejiunga na Simba kwenye usajili huu mkubwa kwa mkopo kutoka TP Mazembe na Kahata amesaini miaka miwili akitokea Gor Mahia ya Kenya. Akizungumza na championi Jumamosi, Rage alisema kuwa Kahata na Deo Kanda ni kati ya usajili bora ambao Simba wameufanya na anaamini watakuja kusumbua sana msimu ujao. “Simba imefanya usajili mzuri, ukiangalia walicheza mechi ya kirafiki na wachezaji wale wachezaji wapya, Deo Kanda na Francis Kahata wakikaa vizuri watasumbua sana pale Simba, kwa ubora wa na hilo halina ubishi. “Yaani namna wanavyocheza unaona kabisa hapa kuna kitu ndani yao hivyo wakitumiwa vyema watakuwa msaada kwenye timu hiyo katika mashindano tofauti,” alisema Rage na kuongeza: “Pia kuna Shomary Kapombe aliyekuwa majeruhi naye amerejea kweli, kiwango kimeonekana kuwa cha hali y...

Taifa Stars yajipa kazi ya kushinda Kenya

Image
 TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, jana Jumapili ilishindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani baada ya kutoka sare ya bila kufungana na Kenya katika mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (Chan). Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ulishuhudiwa na mashabiki wachache waliojitokeza uwanjani hapo. Stars ililisakama lango la Kenya kwa muda mrefu na kipindi cha kwanza kilimalizika wakiwa wanaongoza umiliki kwa 60/40 lakini hawakuweza kuwa na makali ya kufunga bao. Stars ilipata nafasi tatu za wazi katika kipindi cha kwanza lakini ilishindwa kuzitumia vizuri kupata bao. Kipindi cha pili, Stars walifanya mabadiliko kwa kumtoa Ayoub Lyanga na kumuingiza Ibrahim Ajibu dakika ya 54, pia walimtoa Hassan Dilunga wakamuingiza Kelvin John dakika ya 66 lakini hawakuweza kubadili kitu. Dakika ya 84 Stars walifanya mabadiliko tena kwa kumtoa John Bocco na kumuingiza Salim Aiyee lakini bado hawakuweza ...

FEI TOTO AJIKABIDHI AZAM FC

Image
KIUNGO tegemeo wa Yanga, Feisal Salum ‘ Fei Toto’ , amejikabidhi rasmi Azam FC, baada ya kusema klabu hiyo imekuwa ikimwinda kwa muda mrefu na kwamba yupo tayari kutua kama wataafi kiana na Yanga wanaommiliki kwa sasa. Fei Toto alijiunga na Yanga msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Singida United, ambapo tangu atue klabuni hapo, amekuwa ni mmoja wa wachezaji wenye mvuto mkubwa kwa mashabiki wake, hivyo kama ikitokea akachukuliwa na Azam, ataacha simanzi nzito kwao. Akizungumza na Championi Ijumaa, Fei Toto alisema ni kweli Azam wamekuwa wakimfuatilia muda mrefu hivyo kwa kuwa msimu huu unaelekea ukingoni, yeye yupo tayari kutua Azam ikiwa watatimiza vigezo na masharti ya uhamisho kutoka Yanga. “Sina tatizo la kujiunga na Azam maana wamekuwa wakinifuatilia kwa muda mrefu, lakini mbali na hilo mimi kama mchezaji siwezi kuchagua timu ya kuchezea, zaidi naangalia maisha yangu hasa kwa sasa ambapo umri wangu bado ni sahihi kutafuta maisha bora,” alisema. Ch...

SIRI YA POGBA KUHAMA YAFICHUKA

Image
Paul Pogba WAKALA Mino Raiola imebainika ndio chanzo cha Paul Pogba cha kutaka kuondoka Manchester United. Staa wa zamani wa Tottenham na timu ya Taifa ya Misri, Ahmed Hossam `Mido’ alisema anafahamu kuwa wakala Raiola ndio anamvuruga Pogba kiasi cha kushikilia kutaka kuondoka msimu huu. Mido, ambaye alifanya kazi na Raiola kwa kipindi cha miaka 10, alisema anafahamu kuwa Raiola atakuwa bize akisaka timu ya kumnunua Pogba. Manchester United haina mpango wa kumuuza kiungo huyo ingawa kumekuwa na taarifa kuwa Pogba mwenyewe anashinikiza aondoke. Real Madrid kwa muda mrefu sasa inahusishwa kama timu ambayo inataka kumsajili Pogba na Mido amefichua kuwa wakala huyo atakuwa anafanya mambo yake chini kwa chini. “Wakala wa Pogba ni Mino Raiola na mimi nimefanya kazi na Mino, ambaye alikuwa wakala wangu kwa miaka 10 kwa hiyo nafahamu vizuri namna anavyofanya kazi,” alisema Mido. Mido alisema kuwa Raiola atakuwa ameshapiga hesabu zake na kuamini sasa ni wakati muafaka wa ...

Coastal Union kuikazia Simba leo

Image
KOCHA wa Coastal Union, Juma Mgunda amesema kuwa wamejipanga kupata matokeo chanya kwenye mchezo wao wa leo dhidi ya Simba utakaochezwa Uwanja wa Uhuru. Coastal Union wana kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani kwa kufungwa mabao 2-1 hali iliyowafanya wapoteze pointi tatu wakiwa nyumbani. Akizungumza na Championi Jumatano, Mgunda alisema; “Ninaitambua Simba ni timu kubwa na wana wachezaji wenye uzefu ila hilo hainipi taabu kwa kuwa ni timu inayofungika na mbinu zao tayari nimeshazijua.” “Nimewapa kazi ngumu mabeki kuzuia kasi ya mashambulizi ya Simba na pia nimewapa kazi ngumu washambuliaji kuliandama lango la mpinzani lengo ni kupata pointi tatu, mashabiki sapoti ni muhimu,” alisema Mgunda. Coastal Union imecheza jumla ya michezo 33 ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi zao 41 huku Simba ikiwa nafasi ya pili baada ya kucheza michezo 30 ina pointi 78.

ALIYEITUNGUA SIMBA AKARIBIA KUTUA YANGA SC

Image
UNAMKUMBUKA yule winga matata aliyemchambua beki wa Simba, Zana Coulibaly na kutupia? anaitwa Hassan Kabunda wa KMC, unaambiwa anakaribia kutua Yanga. Kabunda alimchambua Coulibaly na kufunga bao la kusawazisha katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza ambao ulimalizika kwa Simba kushinda mabao 2-1. Katika mchezo huo, tofauti na bao hilo winga huyo mwenye kasi alionekana mwiba katika kutokana na kiwango alichokionyesha. Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano, tayari Yanga imeanza kufanya mazungumzo ya awali na winga huyo aliyewahi kuwaniwa na Simba. “Muda mrefu kocha Mwinyi Zahera amekuwa akiomba mawinga wawili wa kushoto na kulia wenye uwezo mkubwa wa kupiga krosi na kasi wakiwa ndani ya uwanja. “Katika mahitaji yake hayo Kabunda ni mmoja wa wachezaji ambao amewataja na viongozi wameridhishwa na uwezo wao wa ndani ya uwanja na kikubwa kinachokwamisha hivi sasa ni suala la fedha. “Hivyo, kama mambo yatakwenda...

AMUNIKE ATANGAZA CHA STARS AFCON

Image
Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kilichotangazwa na Kocha Emmanuel Amunike kwa ajili ya mashindano ya AFCON na CHAN.

STRAIKA MKENYA MAMBO SAFI YANGA

Image
DIRISHA la usajili likifunguliwa, Yanga huenda ikafanya kazi moja tu kutangaza orodha ya kikosi chake na watakapopiga kambi. Kama mambo yakienda sawa huenda kabla ya Ligi haijamalizika wakatangaza kabisa wanaoachwa bila kupepesa macho. Kocha Mwinyi Zahera amemalizana na kiungo mshambuliaji wa Kati wa Kariobang Sharks ya Kenya, Duke Abuya. Mchezaji huyo mwenye umbo kubwa na machachari amemwaga wino kwenye mkataba wa miaka miwili mbele ya Mwinyi Zahera. Abuya aliichapa Yanga mabao mawili katika mchezo wa robo fainali ya Mashindano ya SportPesa ambapo Wakenya hao walishinda mabao 3-2 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Januari 22, mwaka huu. Chanzo makini kutoka ndani ya Yanga kimeeleza kuwa, tayari kocha wao Mwinyi Zahera ameshamalizana na kiungo huyo na kilichobaki ni kutua nchini kwa ajili ya kutambulishwa rasmi kwa mashabiki. “Kocha ameshamalizana na kiungo mshambuliaji wa Kariobang Sharks ya Kenya, Duke Abuya ambaye ameingia mkataba wa miaka miwili na kwamb...

SIMBA SC YAIFANYIA UMAFIA YANGA SC

Image
IMBA imeingia kwenye anga za Yanga, baada ya kocha Patrick Aussems kumfukuzia beki anayewaniwa na vinara hao wa Ligi Kuu Bara. Wekundu wa Msimbazi, juzi Jumamosi walitupwa nje ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuchapwa 4-1 na TP Mazembe mjini Lubumbashi, na sasa hasira zao wanazihamishia kwenye Ligi Kuu Bara ili wapate nafasi nyingine ya kucheza Ligi ya Mabingwa mwakani. Tayari uongozi wa Simba umeshaanza mikakati ya kuwasaka wachezaji wakubwa ili wawe na nguvu zaidi msimu ujao wa Ligi ya Mabingwa, na wanataka wavuke hatua ya robo fainali ambayo wamekomea msimu huu. “Tumejifunza vitu vingi hadi hatua hii ambayo tumefikia na kutolewa. Tumeona kwamba ili usonge mbele kwenye hatua kubwa ni lazima uwe na wachezaji wenye viwango vikubwa na sisi kwa mwakani tutalifanyia kazi hilo,” alisema jana Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori. Kocha Patrick Aussems. Baada ya mechi hiyo ya ambayo ilichezwa huko Lubumbashi nchini DR Congo na Simba kufungwa mabao 4-1, kocha m...

OKWI AWEKA REKODI YA DAKIKA 270 SIMBA

Image
SIMBA ilicheza kwa dakika 270 katika Ligi ya Mabingwa ugenini hatua ya makundi bila ya kufunga bao lolote kabla ya straika Emmanuel Okwi, juzi kufunga katika robo fainali na kuweka rekodi ya kipekee. Okwi ameweka rekodi ya kuwa mfungaji pekee wa Simba ugenini kwenye mechi za tangu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya timu hiyo kucheza dakika 270, sawa na mechi tatu bila kufunga bao lolote. Mganda huyo alifunga bao hilo mbele ya TP Mazembe katika mechi ya pili ya robo fainali ya kombe hilo ambapo Simba walifungwa kwa mabao 4-1 na kutolewa. Kabla Okwi hajafunga, hakukuwa na mchezaji mwingine wa Simba ambaye alifunga bao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ugenini tangu hatua ya makundi. Simba katika mechi zake za ugenini kuanzia hatua ya makundi, walicheza na Al Ahly wakafungwa 5-0, AS Vita 5-0 na JS Saoura 2-0.

AJIBU AONDOLEWA RASMI YANGA…KISA KIPO HAPA

Image
Ibrahim Ajibu HABARI za moto zinazosambaa kwa kasi kwenye ulimwengu wa michezo ni kuwa inadaiwa Klabu ya Yanga imeamua kuchukua maamuzi magumu na kumuondoa kikosini nahodha wake, Ibrahim Ajibu kutokana na kuwepo kwa taarifa kadhaa tata juu yake. Inaelezwa kuwa sababu kubwa ya kuchukuliwa kwa maamuzi hayo ni kudaiwa kuwa kuna ‘mgomo baridi’ ambao staa huyo amekuwa akiufanya kiasi cha kuhusishwa kuwa ni njia ya yeye kushinikiza aongezewe mkataba. Takribani wiki tatu sasa, Ajibu amekuwa nje ya kikosi hicho ikielezwa kuwa amekuwa akisumbuliwa na majeraha, jambo ambalo limekuwa gumu kuaminika kwa mashabiki na baadhi ya viongozi wa Yanga wakiamini kuna sababu nyuma ya kukosekana kwake uwanjani. Chanzo cha habari kimelieleza gazeti hili hivi: “Tayari viongozi wetu wameshamshtukia Ajibu juu ya janja yake ya kugoma kuisaidia timu katika michezo inayoendelea ili ashinikize kupewa mkataba mpya kwa kiwango anachotaka yeye, la sivyo aachwe na aende kuitumikia Simba msimu ujao. “H...

YANGA WAPEWA SH BILIONI MOJA KUTOKA MAREKANI, NA UINGEREZA

Image
UNAWEZA kusema rasmi kamati ya uhamasishaji wa kuichangia Yanga, iliyozinduliwa Aprili 6, mwaka huu ndani ya Morena Hoteli mjini Dodoma, ambayo iko chini ya Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde, imeeleweka ambapo Watanzania waishio nchi za Marekani, Dubai na Uingereza wameichangia Sh bilioni moja. Michango hiyo inajumuisha Watanzania wanaotoka katika nchi nane maarufu kama Diaspora ambazo kwa pamoja zimeunda group la WhatsApp na kuipokea kwa kishindo kampeni hiyo, kiasi cha kuhamasishana mara moja na kuanza michango ambayo hadi sasa inadaiwa kukusanya zaidi ya kiasi hicho. Katibu wa Kamati ya Uchangiaji ya Yanga, mhandisi Deo Mutta, alisema mara baada ya kuizindua rasmi kampeni hiyo, Jumatatu iliyopita aliunganishwa katika group la Watanzania hao na kumpatia mikakati yao huku wakiomba akaunti rasmi watakayotuma fedha za mchango wao. “Kwa makadirio ya haraka hadi sasa hivi nimeona takribani dola mia tano na zaidi zimeshachangwa k...

TAIFA STARS VS SENEGAL, ALGERIA AFCON, MAKUNDI YAPO HAPA

Image
TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imepangwa Kundi C Kwenye michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon 2019) inayotarajiwa kuanza Juni 21 hadi Julai 19, mwaka huu. Droo ya makundi hayo ilichezeshwa jana usiku katika Mji wa Giza uliopo nchini Misri ambapo michuano hiyo ya 32 kwa mwaka huu inafanyika nchini humo. Katika kundi hilo, Taifa Stars imepangwa na Senegal, Algeria na Kenya, ambapo kwa mujibu wa ratiba ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf), Taifa Stars itaanza kucheza dhidi ya Senegal, kisha Algeria na kumaliza na Kenya. Hii ni mara ya pili kwa Taifa Stars kushiriki michuano hiyo, mara ya kwanza ilikuwa 1980 ambapo ilipangwa na timu za Guinea, Morocco na wenyeji Nigeria. Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia na Kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike, walikuwa miongoni mwa wageni waalikwa walioshuhudia tukio hilo la kupangwa makundi.

MAN CITY YAPIGWA NA SPURS UGENINI BAO 1-0

Image
TOTTENHAM Hotspur wakiwa kwenye uwanja wao mpya wa London, jana walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Man City kwenye kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Awali wengi waliamini kuwa Man City wana nafasi kubwa ya kushinda mchezo huu lakini mambo yakawa magumu kwao na kujikuta wakifungwa bao pekee katika dakika ya 78. Katika mchezo huo ambao kila timu ilitawala kwa wakati wake, Son alikuwa shujaa baada ya kuifungia Spurs bao hilo muhimu na likiwa ni la kwanza kwao la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye uwanja wao mpya. City walipata penalti ya utata mwanzoni tu mwa mchezo huo, lakini mshambuliaji wake Sergio kun Aguero shuti lake likapanguliwa na kipa wa Spurs, Hugo Lloris. Mwamuzi wa mchezo huo ilibidi atumie VAR kufahamu kama ni penalti au la baada ya Danny Rose kuunawa mpira kwenye eneo la hatari. Hata hivyo, baada ya penalti hiyo bado timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamu huku City wakikosa nafasi nyingi za wazi. T...