Rage: Kwa Deo Kanda, Kahata Simba SC Imelamba Dume
ISMAIL Aden Rage ambaye ni mwenyekiti wa zamani wa Simba, ameweka wazi kuwa timu hiyo imelamba dume kwa kuwasajili mshambuliaji Deo Kanda na kiungo Francis Kahata.
Deo Kanda amejiunga na Simba kwenye usajili huu mkubwa kwa mkopo kutoka TP Mazembe na Kahata amesaini miaka miwili akitokea Gor Mahia ya Kenya.
Akizungumza na championi Jumamosi, Rage alisema kuwa Kahata na Deo Kanda ni kati ya usajili bora ambao Simba wameufanya na anaamini watakuja kusumbua sana msimu ujao.
“Simba imefanya usajili mzuri, ukiangalia walicheza mechi ya kirafiki na wachezaji wale wachezaji wapya, Deo Kanda na Francis Kahata wakikaa vizuri watasumbua sana pale Simba, kwa ubora wa na hilo halina ubishi.
“Yaani namna wanavyocheza unaona kabisa hapa kuna kitu ndani yao hivyo wakitumiwa vyema watakuwa msaada kwenye timu hiyo katika mashindano tofauti,” alisema Rage na kuongeza:
“Pia kuna Shomary Kapombe aliyekuwa majeruhi naye amerejea kweli, kiwango kimeonekana kuwa cha hali ya juu na akiongeza bidii basi Simba tutaendelea kutesa kama kawaida,” alisema Rage.
Comments
Post a Comment