YANGA WAPEWA SH BILIONI MOJA KUTOKA MAREKANI, NA UINGEREZA



UNAWEZA kusema rasmi kamati ya uhamasishaji wa kuichangia Yanga, iliyozinduliwa Aprili 6, mwaka huu ndani ya Morena Hoteli mjini Dodoma, ambayo iko chini ya Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde, imeeleweka ambapo Watanzania waishio nchi za Marekani, Dubai na Uingereza wameichangia Sh bilioni moja.

Michango hiyo inajumuisha Watanzania wanaotoka katika nchi nane maarufu kama Diaspora ambazo kwa pamoja zimeunda group la WhatsApp na kuipokea kwa kishindo kampeni hiyo, kiasi cha kuhamasishana mara moja na kuanza michango ambayo hadi sasa inadaiwa kukusanya zaidi ya kiasi hicho.

Katibu wa Kamati ya Uchangiaji ya Yanga, mhandisi Deo Mutta, alisema mara baada ya kuizindua rasmi kampeni hiyo, Jumatatu iliyopita aliunganishwa katika group la Watanzania hao na kumpatia mikakati yao huku wakiomba akaunti rasmi watakayotuma fedha za mchango wao.

“Kwa makadirio ya haraka hadi sasa hivi nimeona takribani dola mia tano na zaidi zimeshachangwa kupitia group hilo, na nchi ambazo zimo ni pamoja na Marekani, Saudia, Uingereza, Uturuki, Sweden na Dubai na hizi ni kati ya nchi nane ambazo ninaziona katika group hilo, lakini kwa hamasa ambayo wanayo bado wanazidi kuhamasishana hata katika nchi nyingine zaidi ili zijiunge katika kampeni hiyo.

“Ni matumaini yangu kampeni hii inaonyesha mafanikio makubwa na kwamba siku si nyingi tutavunja lengo kwani hata lengo la kwanza katika uzinduzi wetu wa Dodoma tulilivuka, tulipanga kuanza kuchangisha katika uzinduzi huo Sh milioni 300 lakini siku hiyo kupitia ahadi tulifi kisha Sh milioni 600 na kitu,” alisema Mutta.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!