MAN CITY YAPIGWA NA SPURS UGENINI BAO 1-0



TOTTENHAM Hotspur wakiwa kwenye uwanja wao mpya wa London, jana walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Man City kwenye kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Awali wengi waliamini kuwa Man City wana nafasi kubwa ya kushinda mchezo huu lakini mambo yakawa magumu kwao na kujikuta wakifungwa bao pekee katika dakika ya 78.
Katika mchezo huo ambao kila timu ilitawala kwa wakati wake, Son alikuwa shujaa baada ya kuifungia Spurs bao hilo muhimu na likiwa ni la kwanza kwao la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye uwanja wao mpya.

City walipata penalti ya utata mwanzoni tu mwa mchezo huo, lakini mshambuliaji wake Sergio kun Aguero shuti lake likapanguliwa na kipa wa Spurs, Hugo Lloris.
Mwamuzi wa mchezo huo ilibidi atumie VAR kufahamu kama ni penalti au la baada ya Danny Rose kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Hata hivyo, baada ya penalti hiyo bado timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamu huku City wakikosa nafasi nyingi za wazi.
Timu hizi zitarudiana Jumatano ijayo kwenye Dimba la Etihad na mshindi hapa atakutana na mshindi kati ya
Juventus na Ajax wanaocheza mechi ya kwanza leo.
Tottenham (4-2-3-1): Lloris 8; Trippier 6.5, Alderweireld 7, Vertonghen 6.5, Rose 7; Sissoko 7, Winks 7.5 (Wanyama 80), Eriksen 6.5; Dele Alli 7.5 (Llorente 85), Son 7.5, Kane 7 (Moura 58, 6).
Subs not used: Gazzaniga, Davies, Sanchez, Foyth.
Manager: Mauricio Pochettino 7.5
Scorers: Son 78
Booked: Rose
Manchester City 4-3-3: Ederson 6.5; Walker 6.5, Laporte 6, Otamendi 6, Delph 5.5; Fernandinho 6.5, Gundogan 6.5, D Silva 6.5 (De Bruyne 89); Mahrez 5.5 (Sane 89), Aguero 5.5 (Jesus 71, 6), Sterling 7.
Subs not used: Muric, Kompany, Stones, Foden.
Booked: Laporte, Mahrez
Manager: Pep Guardiola 6.5
Referee: Bjorn Kuipers (Hol)
Attendance: 60,044
Player ratings by Sami Mokbel

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!