OKWI AWEKA REKODI YA DAKIKA 270 SIMBA



SIMBA ilicheza kwa dakika 270 katika Ligi ya Mabingwa ugenini hatua ya makundi bila ya kufunga bao lolote kabla ya straika Emmanuel Okwi, juzi kufunga katika robo fainali na kuweka rekodi ya kipekee.

Okwi ameweka rekodi ya kuwa mfungaji pekee wa Simba ugenini kwenye mechi za tangu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya timu hiyo kucheza dakika 270, sawa na mechi tatu bila kufunga bao lolote.

Mganda huyo alifunga bao hilo mbele ya TP Mazembe katika mechi ya pili ya robo fainali ya kombe hilo ambapo Simba walifungwa kwa mabao 4-1 na kutolewa.

Kabla Okwi hajafunga, hakukuwa na mchezaji mwingine wa Simba ambaye alifunga bao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ugenini tangu hatua ya makundi. Simba katika mechi zake za ugenini kuanzia hatua ya makundi, walicheza na Al Ahly wakafungwa 5-0, AS Vita 5-0 na JS Saoura 2-0.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!