TAIFA STARS VS SENEGAL, ALGERIA AFCON, MAKUNDI YAPO HAPA



TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imepangwa Kundi C Kwenye michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon 2019) inayotarajiwa kuanza Juni 21 hadi Julai 19, mwaka huu.

Droo ya makundi hayo ilichezeshwa jana usiku katika Mji wa Giza uliopo nchini Misri ambapo michuano hiyo ya 32 kwa mwaka huu inafanyika nchini humo.
Katika kundi hilo, Taifa Stars imepangwa na Senegal, Algeria na Kenya, ambapo kwa mujibu wa ratiba ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf), Taifa Stars itaanza kucheza dhidi ya Senegal, kisha Algeria na kumaliza na Kenya.

Hii ni mara ya pili kwa Taifa Stars kushiriki michuano hiyo, mara ya kwanza ilikuwa 1980 ambapo ilipangwa na timu za Guinea, Morocco na wenyeji Nigeria. Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia na Kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike, walikuwa miongoni mwa wageni waalikwa walioshuhudia tukio hilo la kupangwa makundi.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!