CHIRWA ABAKI DAR KWENYE MECHI YAO NA SHELISHELI
Kikosi cha Yanga kimeondoka asubuhi ya leo jijini Dar es Salaam kwenda Shelishli kwa ajili ya mchezo wa marudiano hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Saint Louis Suns utakaofanyika Jumatano mjini humo. Safari hiyo imekuja huku mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa akilazimika kubaki Dar kutokana na kuwa majeruhi. Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amesema Chirwa pamoja na kiungo Thabani Kamusoko na mshambuliaji Donald Ngoma hawajasafiri kutokana na kutokuwa fiti kiafya. Wachezaji wengine majeruhi ambao nao hawajasafiri ni beki Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na mshambuliaji Mrundi Amissi Tambwe. Kikosi cha kamili cha Yanga kilichopondoka leo asubuhi ni: Makipa: Ramadhani Kabwili, Beno Kakolanya na Youthe Rostand. Mabeki: Hassan Kessy, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Gardiel Michael, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Patto Ngonyani na Kelvin Yondani. Viungo: Said Juma ‘Makapu’, Papy Kabamba Tshishimbi, Pius Buswita, Raphael Daud, Yussuf Mhilu, Ibrahim Ajib, Said Muss...