Okwi awafanyia mauaji Ruvu Shooting
Mshambuliaji Emmanuel Okwi ameendeleza rekodi yake tamu dhidi ya Ruvu Shooting baada ya leo kufumania nyavu mara tatu 'hat tricks' katika ushindi wa mabao 5-0 ambao Simba wameupata kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Okwi alifunga mabao hayo katika dakika ya nane, dakika ya 53 na ile ya 77 katika mechi hiyo na kukaribia kurudia kile alichokifanya msimu uliopita alipowafunga Maafande hao mabao manne peke yake kwenye ushindi wa mabao 7-0 ambao Simba ilipata kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi.
Katika mchezo huo uliotawaliwa zaidi na Simba, mabao mengine yalifungwa na Meddie Kagere na Adam Salamba.

Washambuliaji Emmanuel Okwi, Meddie Kagere na John Bocco leo walianza pamoja katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha Simba ikiwa ni baada ya mechi tano kupita tangu walipoanzishwa hivyo.
Wachgezaji hao watatu mara ya mwisho walianzishwa kwenye kikosi cha kwanza Septemba 15 kwenye mchezo wa ugenini dhidi ya Ndanda ambao ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.
Tangu hapo Simba ilicheza dhidi ya Mbao FC, Mwadui FC, Yanga, African Lyon, Stand United na Alliance FC bila watatu hao kuanza pamoja.
Katika kikosi cha kwanza kilichoanza leo dhidi ya Ruvu Shooting, Simba imefanya mabadiliko kadhaa kutoka kwenye kikosi chake kilichoanza ambacho kiliibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Alliance kwa kuwaweka benchi Said Ndemla, Nicholas Gyan, Asante Kwasi, Mohammed Ibrahim na Adam Salamba huku ambao nafasi zao zimechukuliwa na Bocco, Shomary Kapombe, Mohammed Hussein, Shiza Kichuya, Kagere na Jonas Mkude.

Kikosi kilichoanza cha Simba ni Aishi Manula, Kapombe, Mohammed Hussein, Paschal Wawa, Juuko Murshid, Mkude, Okwi, Cletus Chama, Shiza Kichuya, Bocco, Kagere.
Kikosi cha Ruvu Shooting kinaundwa na wachezaji Abdallah Rashid, Abdul Mpambika, Mau Bofu, Renatus Ambrose,Tumba Swedi, Zuberi Dabi, Shaban Usala, Baraka Mtuwi, Said Dilunga, Fully Maganga, William Patrick
Comments
Post a Comment