CANNAVARO APEWA KUKU
BEKI na nahodha wa zamani wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, jana alifanyiwa ‘sapraiz’ ya kutosha kutoka kwa mashabiki wa Yanga kutoka Kijiji cha Chigungu kilichopo Masasi mkoani Mtwara.
Mashabiki hao walikuwa barabarani kuusubiri msafara wa Cannavaro ambaye kwa sasa ni meneja wa Yanga uliokuwa unaenda Mtwara kufungua Tawi la Yanga.
Msafara huo ukiwa njiani, ulisimamishwa na mashabiki hao ambapo wazee wa eneo hilo walimkabidhi Cannavaro katoni nne za maji huku wakimwambia akirudi apitie kuchukua kuku wake kama zawadi.
Comments
Post a Comment